Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini kimeamua kufungua kesi mahakamani kwenda kuwashtaki Wasimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa, Wasimamizi Wasaidizi pamoja na walioshinda na kuapishwa katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024
Hayo yamesemwa na Kiongozi Mstaafu wa chama hicho Zitto Kabwe wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wafuasi wa chama hicho pamoja na wananchi wa Kigoma waliojitokeza kumsikiliza jana Novemba 29, katika Uwanja wa Kawawa, uliopo Ujiji Kigoma.
PIA SOMA
- LGE2024 - ACT Wazalendo: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ubatilishwe na kuitishwa upya