Kigoma: Anayetuhumiwa kuua watu 7 wa familia moja apandishwa Kizimbani

Kigoma: Anayetuhumiwa kuua watu 7 wa familia moja apandishwa Kizimbani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mshtakiwa wa kesi ya mauaji ya watu saba wa familia moja, yalitokea katika kijiji cha Kiganza mkoani hapa, Peter Moris (33), amefikishwa katika Mahakama KuuKanda ya Kigoma, kwa mara ya kwanza na kusomewa maelezo ya kosa ambapo alikana kuhusika na tukio hilo.

Akisomewa maelezo hayo leo Februari 6, 2023, mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Lameck Mlacha na wakili wa Serikali, Edna Makala amedai, mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa saba ya kuua kwa kukusudia kinyume cha kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Amedai kuwa mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Julai 3, 2022, huko katika kijiji cha Kiganza, wilayani Kigoma, mkoani Kigoma, aliwaua watu saba kwa kuwakata na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao.
“Katika kesi kwa upande wa mashitaka tunatarajia kuleta mahakamani hapa mashahidi 23 na vielelezo 12 ikiwemo nguo aina ya tisheti moja, suruali ya jinsi moja nguo za mshtakiwa, taarifa ya mkemia mkuu wa serikali na panga moja,” amesema wakili Makala.

Kwa upande wake wakili wa upande wa utetezi, Sadiki Aliki amesema mshtakiwa atajitetea akiwa chini ya kiapo na kwamba kwasasa hawatatoa mashahidi wala vielelezo kwa upande wao.

Wakili Aliki amesema endapo watakuwa na vielelezo na mashahidi kwa upande wao basi watavitoa mahakamani hapo kwa kufata utaratibu wa kisheria.

Baada ya kukamilika kwa usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo, Jaji Mlacha ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe itakayopangwa na naibu msajili wa mahakama hiyo ambapo itafuata hatua ya usikilizwaji wa mashahidi.

Ikumbukwe mshtakiwa huyo alitekeleza mauaji hayo Julai3, mwaka 2022 katika kijiji cha Kiganza, wilayani Kigoma na Julai4, 2022 alikamatwa maeneo ya Mwanga, Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwa amevaa tisheti na suruali ikiwa na madoa ya damu.

Waliouawa katika tukio hilo ni Tilifera Toyi (70),Januari Mussa(35), Joel Mussa(40), Sara Dunia(28) ambaye ni mke wa Januari , Christina Lazaro(9), James Joel (7) na James Januari(4) aliyefariki akiwa njiani kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

MWANANCHI

Pia soma:

 
Back
Top Bottom