Kigoma: Auawa kwa kukatwa shingo, wauaji waondoka na kichwa

Kigoma: Auawa kwa kukatwa shingo, wauaji waondoka na kichwa

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Janda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma aliyetambulika kwa jina Shinze Mugarama ameuawa kwa kukatwa shingo kijijini hapo na wauaji kuondoka na kichwa chake.

Screenshot_20210411-171030.jpg

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi James Manyama amesema marehemu ambaye hana familia na makazi maalum kijijini hapo amekutwa na mkasa huo baada ya kuomba hifadhi ya kulala kwa siku hiyo nyumbani kwa Bw. Juma Zegeli na kwamba watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Aidha, Kamanda Manyama amesema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa familia yake ambapo ametoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom