Pre GE2025 Kigoma kuuziwa majiko banifu ya ruzuku kwa Tsh. 10,000

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
KIGOMA: MAMA lishe na walengwa wa kusaidia kaya masikini Manispaa ya Kigoma Ujiji wanatarajia kunufaika na ugawaji wa majiko banifu yaliyogaiwa na Mamlaka ya Nishati Vijijini (REA) kuhamasisha matumizi ya nishati safi na utunzaji mazingira


Makundi hayo yatanufaika na ruzuku ya 80% ya majiko banifu 200,000 ambapo badala ya kununua jiko moja Sh 55,000 watapata ruzuku ya serikali kwa kununua jiko moja 10,000.

Joseph Sambali mtaalam wa nishati na masuala ya jinsia kutoka Wakala wa Nishati Vijiji (REA) anaeleza.



Akizungumza leo Machi 7, 2025, katika hafla ya kugawa bure majiko 400 kwa mama lishe na walengwa wa kusaidia kaya masikini (TASAF), Joseph Sambali amesema hatua hiyo ni uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi katika kutekeleza mpango wa serikali wa asilimia 90 ya watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034.

Ametaja vipaumbele wa wanufaika kuwa ni makundi maalum hasa vijijini ambako matumizi ya kuni na mkaa ni makubwa.

Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

 
Hamna jiko humu
 
Si muwape mitungi ya gesi Au Huko mama Samia hawajui.
 
Kwanini isiwe gas kwa tsh 10k
 
Hayo majiko kwa mama ntilie ni hasara, yanapika slow Sana si wangewapa tu mitungi ya gasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…