Pre GE2025 Kigoma: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Kigoma: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kigoma. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Kigomaa.jpg

Kigoma ni mkoa uliopo magharibi mwa Tanzania, ukipakana na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa upande wa magharibi na kaskazini. Mkoa huu unajulikana kwa ziwa la Tanganyika, ambalo ni moja ya maziwa marefu zaidi duniani.

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA KIGOMA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya Watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Kigoma ni 2,470,967; wanaume 1,186,833 na wanawake 1,284,134, ikiwa na wilaya 5.

Idadi ya Majimbo ya Mkoa wa Kigoma
Mkoa wa Kigoma una majimbo Nane ya uchaguzi
  • Jimbo la Buyungu
  • Jimbo la Kasulu Mjini
  • Jimbo la Kasulu Vijijini
  • Jimbo la Kigoma Kaskazini
  • Jimbo la Kigoma Kusini
  • Jimbo la Kigoma Mjini
  • Jimbo la Buhigwe
  • Jimbo la Muhambwe
ILIVYOKUWA UCHAGUZI MKUU 2020

Katika uchaguzi mkuu wa 2020 mkoani Kigoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishinda kwa kiwango kikubwa katika ngazi zote.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hayati John Magufuli alipata kura nyingi katika mkoa huu kwenye nafasi ya urais, akipata zaidi ya asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Katika nafasi za ubunge, wagombea wa CCM walishinda viti vyote vya majimbo, huku ACT Wazalendo ikipoteza ngome jimbo la Kigoma mjini.

Aidha, kwenye udiwani, CCM ilijinyakulia kata takriban zote kutokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Updates

January

February
March
ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom