LGE2024 Kigoma: Mgombea ACT aahidi sherehe ya ushindi baada ya uchaguzi

LGE2024 Kigoma: Mgombea ACT aahidi sherehe ya ushindi baada ya uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kuna tafrija huko tumeandaliwa mapochopocho tukajirushe.

====

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji cha Nyamsanze, kata ya Buhoro, wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zedekia Mathias, ameahidi kuandaa tafrija nyumbani kwake kusherehekea ushindi atakaoupata baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Zedekia, akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, amesema kuwa uhusiano mzuri aliojenga na wakazi wa Nyamsanze, pamoja na uchapakazi na mapenzi yake kwa kijiji hicho, vinampa uhakika wa kupata ushindi.

Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mgombea huyo pia ameahidi kushirikiana na wananchi katika kuimarisha maendeleo ya kijiji kupitia miradi mbalimbali ya kijamii baada ya uchaguzi.
 
Bora huyo wananchi tutafaidi hata wali kuliko kukosa vyote baadae. Maana wanasiasa tunawajua
 
Back
Top Bottom