Kuna tafrija huko tumeandaliwa mapochopocho tukajirushe.
====
Your browser is not able to display this video.
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji cha Nyamsanze, kata ya Buhoro, wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zedekia Mathias, ameahidi kuandaa tafrija nyumbani kwake kusherehekea ushindi atakaoupata baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Zedekia, akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, amesema kuwa uhusiano mzuri aliojenga na wakazi wa Nyamsanze, pamoja na uchapakazi na mapenzi yake kwa kijiji hicho, vinampa uhakika wa kupata ushindi.