Kigoma: Polisi kuchunguza tukio la kutoweka kwa mfanyabiashara Mahamoud Abdalla aliyechukuliwa na watu wasiojulikana

Kigoma: Polisi kuchunguza tukio la kutoweka kwa mfanyabiashara Mahamoud Abdalla aliyechukuliwa na watu wasiojulikana

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Polisi Kigoma.jpg

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetangaza kuanza uchunguzi wa kina kufuatia taarifa za kutoweka kwa mfanyabiashara wa Soko la Buzebazeba, Mahamoud Juma Abdallah (25), anayedaiwa kuchukuliwa na watu wasiofahamika akiwa eneo lake la kazi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Philemon Makungu, Februari 20, 2026, tukio hilo liliripotiwa rasmi Februari 19 majira ya saa 09:00 asubuhi. Mahamoud, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mwasenga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, anadaiwa kutoweka katika mazingira tatanishi akiwa kazini kwake sokoni.

"Uchunguzi utakapokamilika utabaini ukweli wa tuhuma hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa au ushahidi ambao utasaidia uchunguzi kukamilika kwa wakati aufikishe Polisi ili uweze kufanyiwa kazi kwa haraka", imeeleza taarifa hiyo.

Wakati msako na uchunguzi ukiendelea, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma amewataka wakazi wa Kigoma Ujiji na mkoa mzima kwa ujumla kuwa watulivu. Polisi wameahidi kutoa mrejesho mara baada ya ukweli wa tukio hilo kubainika na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wowote
watakaobainika kuhusika na suala hilo.
 
Alikua na mrengo gani wa kisiasa huyo mfanyabishara? maana sasahivi ukiwa mtu wa haki hutakiwi
 
Inaelezwa kwamba amechukuliwa na watu wanaoitwa Wasiojulikana na kupotezwa.

Ikiwa bahati ya mtende basi tutaokota maiti Yale kama tulivyookota ya Bajoo, Au kama ilivyo kawaida itakuwa kwaheri ya kuonana

Lakini Je ni nani anaye injoi kwa watu kuuawa kikatili namna hii hasa mwezi huku Mtukufu?
 
Hawa wanaoteka watu wanamuharibia Mama,na hii ndio itapelekea kushtakiwa ICC! soon atashtakiwa kweli kwa haya yanayoendelea na yeye au wakuu hawakemei kabisa,wapo kimiya tu....
Huu ni upuuzi unachafua Nchi kabisa kabisa....itamghalimu huyu mama....ni suala la muda! Time will tell!!
 
Je ni nani anaamuru haya aliyejuu ya Mama?
 
Sema hii mambo ya kunyakuwa watu kama vifaranga hata kama mtu ana ishu ya kesi ya jinai in long run itakuja kuleta athari mbaya sana. Ni swala la muda tu
 
Nikazane nilipe madeni ya watu!
Sasa hivi mtu hata mkinyimana chumvi uswazi anaweza kukupoteza na hamna mtu atafanya lolote 😭
 
Back
Top Bottom