KERO Responded KIGOMA tunalipia Mita mpya ya Umeme inapounganishwa tunakutana na deni, TANESCO hii ni sawa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wananchi wa Kigoma niliyeamua kuvuta umeme nyumbani kwangu kwa mara ya kwanza kabisa. Nilifanya taratibu zote zinazotakiwa, nikalipia huduma, na juzi tu nikafungiwa mita yangu mpya.

Nilikuwa na furaha sana, nikiamini sasa naanza kutumia umeme kama wengine. Lakini mambo yalibadilika ghafla pale nilipoenda kununua umeme kwa mara ya kwanza. Niliambiwa sina salio la kutosha. Nikashangaa, nikajiuliza inawezekanaje wakati hata sijawahi kutumia umeme?

Nikaamua kupiga simu TANESCO ili kupata ufafanuzi. Walipoangalia mita yangu, wakaniambia kuwa nina deni la shilingi 12,000. Nilishangaa sana. Nikawauliza, hilo deni limetoka wapi wakati hii ni mara yangu ya kwanza kabisa kupata huduma hii?

Kilichoniumiza zaidi ni kwamba niliambiwa ili niweze kununua umeme, lazima kwanza nilipe hilo deni. Na hata nikilipa, bado kutakuwa na makato yanayoendelea katika miezi inayofuata. Hapo ndipo nikazidi kuchanganyikiwa—ina maana nimeanza na mzigo wa deni ambalo silijui lilikotoka?

Nilipoanza kuzungumza na watu wengine mtaani, nikagundua kuwa mimi si peke yangu. Wapo wengi waliokumbana na hali kama hii—wanawekewa mita mpya lakini zinakuja na madeni tayari.

Hali hii inanipa maswali mengi sana:
  • Haya madeni yanatoka wapi?
  • Kwa nini mimi nibebe deni ambalo sijawahi kulisababisha?
  • Ni haki kweli kwa mteja mpya kuanza na deni?
Kwa kweli hali hii inakatisha tamaa. Nilitegemea kuanza maisha mapya ya kutumia umeme kwa furaha, lakini badala yake nimeanza kwa sintofahamu na mzigo usioeleweka.

Naomba mamlaka husika walifuatilie jambo hili kwa haraka na watupatie majibu ya wazi.

Mimi nahitaji haki yangu kama mteja mpya.
===
Majibu ya TANESCO - TANESCO yatolea ufafanuzi wa Kero zilizowasilishwa na Wadau kutoka JamiiForums, hatua za maboresho zimechukuliwa
 
Kodi ya Jengo utasikia.....unskatwa kila mwaka ...!!:
 
Kwa kawaida wateja wapya wanapocheck salio wanakuta kianzio cha kama unit 9 hivi, sasa kama umekuta deni ni ajabu sana na huo utakuwa uhuni wa baadhi ya watendaji wa TANESCO.
 
Ninachokifahamu,
Haya makato Tanesco hawahusiki,

Hii ni kodi ya majengo ambayo serikali wameona njia rahisi wao kuikusanya ni kupitia manunuzi ya umeme ambayo kwa kila mwezi ukinunua umeme wanakata 1500,

Kinachotokea kwa wateja wapya hua wanaanza kuhesabu na kujumlisha hizi 1500 kuanzia mwezi wa serkali(mwezi wa saba) unapoanza.

Hivyo mf umeingiziwa umeme mwezi wa nane,hapa utakua na deni la 3000 yaani july na august.
Thnx!
 
Hii serikali ya chura aka kizimkazi haina huruma na watanganyika tusipo amka cjui itakuaje hapo mbeleni.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom