Kigoma: Ujenzi wa Daraja la Malagarasi unaendelea, Mhandisi asema lina urefu wa Mita 76

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Meneja wa TANROADS Kigoma, Mhandisi Narcis Choma amezungumzia Sehemu ya Tatu ya mradi wa barabara inayoendelea na ujenzi wake Mkoani hapo amegusia pia kuhusu ujenzi wa Daraja la Malagarasi.

Ameeleza kuwa mradi huo unaohusisha barabara ya Mvugwe – Nduta yenye urefu wa Kilometa 59.3, gharama yake ni Tsh. Bilioni 84.7 na ujenzi wake umefikia katika kiwango cha 86%.

Anasema: “Tupo kwenye ujenzi wa Daraja la Malagarasi, mchakato unaendelea, daraja lina urefu wa Mita 76, ndio daraja kubwa kuliko mengine yote katika huu Mradi wa Lot 3

“Mto huu umeanzia kule Manyovu na ukiwa umechukua madaraja mengi ikiwemo Daraja Kikwete na umeelekea Ilagala.”

Kushoto ni Daraja linalotumika sasa na Kulia ni daraja linalojengwa
 
Weka picha wewee
 
Ukiwa Unasoma Kwenye Mitandao Utajua Wanasiasa Hawafai Nimetoka Kigoma Hiyo Njia Kuanzia Kaliua Shimo Mpaka Uvinza Mkandarasi Hafanyi Lolote Mvua Tele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…