Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ni vuta ni kuvute kati ya wananchi wa Kata ya Buhanda, Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, na Shirika la Reli Tanzania (TRC), baada ya baadhi ya wananchi kukataa kusaini tathmini ya fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa-SGR kipande cha sita, Tabora -Kigoma.
Wananchi hao wamedai kuwa fidia waliyopangiwa haiendani na thamani halisi ya mali zao katika kupisha ujenzi wa mradi huo.
Baadhi yao wamesikitishwa na tofauti ya viwango vya fidia kati ya wananchi ndani ya kata hiyo hiyo, huku baadhi wakidai wenzao wamefanyiwa uthamini wa viwango vya juu na wengine wakipewa viwango duni,mabako kumewafanya baadhi ya wananchi kusita kusaini nyaraka za tathmini, wakitaka ufafanuzi wa kina kuhusu vigezo vilivyotumika kufikia viwango hivyo.
Akizungumza kuhusu suala hilo, Mthamini Mkoa wa Kigoma, Oscar Mwanzalila, amesema viwango vya tathmini vimegawanywa katika makundi matatu, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa tofauti za thamani za fidia miongoni mwa wananchi.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Buhanda, Edward Misigaro, amewataka wananchi kuwa watulivu huku akiwahakikishia kuwa kila mmoja atapata haki yake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma ni miongoni mwa miradi inayolenga kuimarisha usafiri wa reli na kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.
Soma pia