LGE2024 Kigoma: Wananchi waipongeza TAMISEMI mchakato Uchaguzi Serikali za Mitaa

LGE2024 Kigoma: Wananchi waipongeza TAMISEMI mchakato Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mbona ghafla kila sehemu wanaanza kuipongeza OR TAMISEMI? Yaani ni kama wote wamepewa script moja :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:, mbinu ni zile zile CCM hamjui kunyumbulika kabisa!

=====



Kupata mijadala kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Wananchi wa mkoa wa Kigoma wamepongeza juhudi za serikali katika kuendelea kutekeleza mchakato wa kuwapata wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika tarehe 27, Novemba, 2024. Wamesema kuwa mchakato huu unatoa fursa kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowaamini watakaowatumikia na kuleta maendeleo katika jamii zao.

Baadhi ya wananchi wamesifu uwazi na umakini wa mchakato wa kuwapata wagombea, wakisema kuwa serikali imeonyesha kujali sauti na mahitaji yao. Wengine wameeleza matumaini yao kwamba uchaguzi huu utaenda vizuri bila kuwepo kwa changamoto za kiusalama na migogoro, na wameiomba serikali kuendelea kuhakikisha kuwa mchakato unafanyika kwa haki na uwazi.
 
Inahitaji ukosefu wa akili wa kiwango cha huu mno kusifia huu uchafuzi wa uchaguzi wa serikali za mitaa
 
watu wote makini wako sambamba na tamisemi

umakini wa Tamisemi umetukuka uliza mtu yoyote asie tumia kimiminika kichwani atakujuza
 
Back
Top Bottom