Wananchi wa mkoa wa Kigoma wamepongeza juhudi za serikali katika kuendelea kutekeleza mchakato wa kuwapata wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika tarehe 27, Novemba, 2024. Wamesema kuwa mchakato huu unatoa fursa kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowaamini watakaowatumikia na kuleta maendeleo katika jamii zao.
Baadhi ya wananchi wamesifu uwazi na umakini wa mchakato wa kuwapata wagombea, wakisema kuwa serikali imeonyesha kujali sauti na mahitaji yao. Wengine wameeleza matumaini yao kwamba uchaguzi huu utaenda vizuri bila kuwepo kwa changamoto za kiusalama na migogoro, na wameiomba serikali kuendelea kuhakikisha kuwa mchakato unafanyika kwa haki na uwazi.