JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Watu tisa Wilayani Kakonko, Kigoma wanashikiliwa kwa kukutwa na viungo vya binadamu ikiwemo mbavu na mguu ambavyo vinadaiwa vilikuwa vikipelekwa Mwanza.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema: “Watuhumiwa walikamatwa katika kizuizi baada ya askari kutilia shaka gari lao T948 DQU lililokuwa limebeba abiria pia.
“Mtuhumiwa mmoja alimtaja mtu mmoja (jina linahifadhiwa) aliyekuwa akimpelekea viungo hivyo Sengerema, Mwanza, baada ya kufuatiliwa walikamatwa.”
Video: Azam TV