Hizi mita za maji zinazoibiwa si dili za watu kadhaa kutoka kwenye mamlaka husika jamani, maana wizi huu umetawala sana.
======
Zaidi ya mita 300 za maji zimeripotiwa kuibwa katika kipindi cha mwaka mmoja mkoani Kigoma. Mkuu wa mkoa huo, Thobias Andengenye ameitaka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), wananchi pamoja na polisi kuendelea kuwasaka na kuweka mikakati madhubiti ya kukabiliana na kukithiri kwa wizi huo.