LGE2024 Kigoma: Zitto apiga kura uchaguzi serikali za mitaa, azungumzia kura bandia kukamatwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, akibainisha kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaoshughulikia changamoto za moja kwa moja katika maeneo yao.

Zitto ametoa wito huo mapema siku ya Jumatano Novemba 27, 2024 baada ya kumaliza kupiga kura katika kitongoji cha Kibingo A, kata ya Mwandiga, jimbo la Kigoma Kaskazini, mkoani Kigoma.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akiwa ameonesha kuridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hicho na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, Zitto aliwataka Watanzania waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura.

Hata hivyo ametoa wito kwa wanaoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kutofanya vitendo vya kuharibu uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo, katika mkoa wa Kigoma kumeripotiwa matukio mbalimbali ikiwamo kukamatwa kwa kura feki, na baadhi ya wagombea kukamatwa.

Amesisitiza kuwa ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi, huku akiwapongeza wale ambao tayari wamepiga kura kwa kuwa mfano mzuri wa uzalendo.
 
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, akibainisha kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaoshughulikia changamoto za moja kwa moja katika maeneo yao.

Uwezo wa TAMISEMI KUSIMAMIA BADO NI MDOGO SANA
 
Back
Top Bottom