Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Kiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amewataka watendaji wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kuacha kukikumbatia chama cha CCM kwani ni chama ambacho kimeshindwa kuwalinda watendaji wa manispaa na watendaji wa kata hivyo katika uchaguzi wa Novemba 27, wasiingize mguu wao uwanjani bali waache vyama vishindane na atakayeshinda ashinde kihalali.
Zitto ametoa wito huo siku ya Jumanne Novemba 26, 2024 wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 2024- 2029 uliofanyika katika uwanja wa Mwanga Community Centre uliopo katika kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Aidha amewahimiza wananchi wa manispaa hiyo kujitokeza kwa wingi kupiga kura, kuzisimamia na kuzilinda mpaka pale mshindi wa halali atakapotangazwa, huku akiwataka kuwa walinzi dhidi ya nyendo zozote mbaya zile zitakazohisiwa kabla ya uchaguzi.
PIA SOMA
- LGE2024 - Zitto Kabwe aonya watakao bebeshwa kura ya ziada, asema yatakayowakuta wasilaumiane "Dua imesomwa, tendeni haki"