KERO Kigongo - Busisi: Hali ya huduma ya vyoo hairidhishi pamoja na wahusika kukusanya mapato

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pamoja na kukusanya mapato kila siku ya shs 500 kupanda kivuko, lakini kuna shilingi 200 kwa kila anayetumia huduma ya vyoo hapa ferry.

Kitu kinachochefua ni huduma mbovu ikiwepo na ubovu wa vyoo, maji hakuna, vyoo vichafu na hazifanyiwi usafi.

Nimeshangazwa sana na hali hii kutokana na mapato ambayo nilimuuliza msimamizi kwa lugha ya investigation akasema pesa inayokusanywa kila siku, kweli ni nyingi.

Mh. Bashungwa nadhani hapa napo kuna haja ya kutuma au kwenda kuangalia, kwanza hawatoi risiti yoyote so pesa sijui inaenda kwa nani?.

Picha hizi hapa.

View attachment 3003517

👆🏾 Ni sehemu ya haja ndogo upande wa wanaumme, hapo nimekutana na nyuki wakitafuta malisho yao pamoja na harufu kali.

View attachment 3003521
👆🏾 Hapo ni sehemu ya kunawa mikono, lakini hapafai hata wao wameona iwe sehemu ya kutunzia kisafisha choo, angalia tiles hapo chini.

View attachment 3003526
👆🏾Hii siyo chai ya maziwa ni maji yaliyopo ndani ya choo hapo kivukoni na hamna chombo cha kuchotea maji, japokuwa maji masafi ya ziwa Victoria yapo hatua 3 hapo nje.
Mtanikimbuka. Huyu waziri ni mpiga Sound sana
 
Kuna choo cha kulipia kipo ktk stendi ya mabasi ya wilaya pale Sikonge,mkoani Tabora,choo ni kichafu sijui ni cha mtu binafsi au cha serikali sijawai ona.
Hata kama mmiliki ni mtu binafsi serikali ilitakiwa kumwajibisha mmiliki wa choo ili aweke mazingira safi lakini hii nchi sijui nani katuloga mabwana afya ufanya kazi pale wanaposikia mgonjwa kafa na kipindupindu ndipo ushituka usingizini.
Hii nchi ina changamoto lukuki lakini nyingi ni za kujitakia, hasa usafi wa vyoo.

Ukiwa katika vivuko vya Nyehunge kutoka Kirumba jijini Mwanza na Kamanga wilayani sengerema, vyoo hya vivuko hivyo ni shida na mbaya zaidi wanaacha maji yanasambaa katika eneo kubwa la kivuko, huku biashara za vitumbua zikiendelea na wauzaji waliovaa kandambili na huwezi kufahamu mara mwisho huo mguu ulioshwa lin.

Unafika Geita unaomba( jambo la ajabu) kwenda kujisaidia, choo cha stendi na afisa amekaa mbele ya meza anachikua fedha kwa wanaojisaidia huko ndani kuchafu!

Ingia, Biharamulo stand, choo kina hali mbaya hasa sehemu ya haja ndogo kwa abiria, watu wanagawana magonjwa!

Unafika Ngara, jioni unapelekwa na mwenyeji wako out, bar maarufu yenye wahudumu wengi kulliko wateja, nenda chooni sasa, duh kwa hakika kwa hali hii ya choo cha wanaume iliyogeuka rangi na kuwa njano huku kukiwa na choo kimoja cha haja kubwa, magonjwa ni nje nje. Mwenyeji anakueleza hapo ndio kijiwe cha maofisa wa serikali na hata mabwana afya!

Unafika Kibondo, baada ya kusimama Nyakanazi kupata supu ya samaki na kupelekwa choo huko uchochoroni ndani unakuta aliyejisaidia mara mwisho wala hakuwa na haja ya kumwaga maji aliacha hivyo hivyo. Sasa uko kibondo.

Unakwenda kibodeko, hapa wametia fora, ukumbuke jengo hili ni mali ya halmashauri, lakini upande wa choo pako hoi.

Watu wanajisaidia mita mbili kuttoka chooni na hilo eneo la mita mbili kutoka chooni limekuwa kama jaruba la mikojo na huku bar ikiwa na watu kama harusi! Wafanyabiashara hawa wanajua kuwakusanya wasichana wengii kuttoka maenek mbalimbali ya nchi.

Sasa ingia kasulu hizo bar mbili zilizoki mkabala ambazo kuna biashara zote za dunia za uzinzi, vyoo vyake ni vichafu na havifai kwa matumizi ya binadamu.

Mifano hii michache ni kieleleZo kuwa maafisa waliopaswa kusimamia usafi nchini walikwishaa poteza sifa za kazi zao lakini wanadai waongezwe mishahara!
 
Tatizo liko hapa kwa hao unaowaita maafisa:
1. Walikulia kwenye hayo mazingira
2. Wakafaulu kwa kukariri majibu na siyo kuelewa
3. Kwa hiyo hawana tofauti na ambao hawajaenda shule.
 
Tatizo liko hapa kwa hao unaowaita maafisa:
1. Walikulia kwenye hayo mazingira
2. Wakafaulubkwa kukariri majibu na siyo kuelewa
3. Kwa hiyo hawana tofauti na ambao hawajaenda shule.
Ukienda mbele kwa mtazamo wako.... nafikiri mpaka nacheka.
Najiuliza wasimamizi wao vipi? Na je huko kwenye makazi yao kukoje?
 
Aahahaa, camaraderie upo lakini?.
Camaraderie😀😀😀
Imebidi nigoogle kwanza maana yake baada ya kuona limefanana na Kikwenu lakini siyo kikwenu!

Nashukuru mkuu kwa kuniongezea msamiati!

Acha nirudierudie, CAMARADERIE ili nisisahau!
 
Camaraderie😀😀😀
Imebidi nigoogle kwanza maana yake baada ya kuona limefanana na Kikwenu lakini siyo kikwenu!

Nashukuru mkuu kwa kujiongezea msamiati!
Acha nirudierudie, CAMARADERIE ili nisisahau!
Hilo neno ni lugha ya kwetu chief ndiyo maana nimelitumia, pia ni kwa sababu, yawezekana ukawa jamaa yangu au usiwe ila kikubwa you have something elsewhere!.
 
Back
Top Bottom