KERO Kigongo - Busisi: Hali ya huduma ya vyoo hairidhishi pamoja na wahusika kukusanya mapato

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mtanikimbuka. Huyu waziri ni mpiga Sound sana
 
Hii nchi ina changamoto lukuki lakini nyingi ni za kujitakia, hasa usafi wa vyoo.

Ukiwa katika vivuko vya Nyehunge kutoka Kirumba jijini Mwanza na Kamanga wilayani sengerema, vyoo hya vivuko hivyo ni shida na mbaya zaidi wanaacha maji yanasambaa katika eneo kubwa la kivuko, huku biashara za vitumbua zikiendelea na wauzaji waliovaa kandambili na huwezi kufahamu mara mwisho huo mguu ulioshwa lin.

Unafika Geita unaomba( jambo la ajabu) kwenda kujisaidia, choo cha stendi na afisa amekaa mbele ya meza anachikua fedha kwa wanaojisaidia huko ndani kuchafu!

Ingia, Biharamulo stand, choo kina hali mbaya hasa sehemu ya haja ndogo kwa abiria, watu wanagawana magonjwa!

Unafika Ngara, jioni unapelekwa na mwenyeji wako out, bar maarufu yenye wahudumu wengi kulliko wateja, nenda chooni sasa, duh kwa hakika kwa hali hii ya choo cha wanaume iliyogeuka rangi na kuwa njano huku kukiwa na choo kimoja cha haja kubwa, magonjwa ni nje nje. Mwenyeji anakueleza hapo ndio kijiwe cha maofisa wa serikali na hata mabwana afya!

Unafika Kibondo, baada ya kusimama Nyakanazi kupata supu ya samaki na kupelekwa choo huko uchochoroni ndani unakuta aliyejisaidia mara mwisho wala hakuwa na haja ya kumwaga maji aliacha hivyo hivyo. Sasa uko kibondo.

Unakwenda kibodeko, hapa wametia fora, ukumbuke jengo hili ni mali ya halmashauri, lakini upande wa choo pako hoi.

Watu wanajisaidia mita mbili kuttoka chooni na hilo eneo la mita mbili kutoka chooni limekuwa kama jaruba la mikojo na huku bar ikiwa na watu kama harusi! Wafanyabiashara hawa wanajua kuwakusanya wasichana wengii kuttoka maenek mbalimbali ya nchi.

Sasa ingia kasulu hizo bar mbili zilizoki mkabala ambazo kuna biashara zote za dunia za uzinzi, vyoo vyake ni vichafu na havifai kwa matumizi ya binadamu.

Mifano hii michache ni kieleleZo kuwa maafisa waliopaswa kusimamia usafi nchini walikwishaa poteza sifa za kazi zao lakini wanadai waongezwe mishahara!
 
Tatizo liko hapa kwa hao unaowaita maafisa:
1. Walikulia kwenye hayo mazingira
2. Wakafaulu kwa kukariri majibu na siyo kuelewa
3. Kwa hiyo hawana tofauti na ambao hawajaenda shule.
 
Tatizo liko hapa kwa hao unaowaita maafisa:
1. Walikulia kwenye hayo mazingira
2. Wakafaulubkwa kukariri majibu na siyo kuelewa
3. Kwa hiyo hawana tofauti na ambao hawajaenda shule.
Ukienda mbele kwa mtazamo wako.... nafikiri mpaka nacheka.
Najiuliza wasimamizi wao vipi? Na je huko kwenye makazi yao kukoje?
 
Aahahaa, camaraderie upo lakini?.
Camaraderie😀😀😀
Imebidi nigoogle kwanza maana yake baada ya kuona limefanana na Kikwenu lakini siyo kikwenu!

Nashukuru mkuu kwa kuniongezea msamiati!

Acha nirudierudie, CAMARADERIE ili nisisahau!
 
Camaraderie😀😀😀
Imebidi nigoogle kwanza maana yake baada ya kuona limefanana na Kikwenu lakini siyo kikwenu!

Nashukuru mkuu kwa kujiongezea msamiati!
Acha nirudierudie, CAMARADERIE ili nisisahau!
Hilo neno ni lugha ya kwetu chief ndiyo maana nimelitumia, pia ni kwa sababu, yawezekana ukawa jamaa yangu au usiwe ila kikubwa you have something elsewhere!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…