Kigonsera sec school

Kigonsera sec school

NaCl

Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
40
Reaction score
3
Jamani nimepangiwa cbg kigonsera huko Ruvuma mi niko Dodoma naombeni msaada wenu kwa wanaifahamu hiyo shule kitaaluma,mazingira na anielekeze nitafika vp
 
Kigonsera kitaaluma ni nzuri, mazingira ni mazuri kujifunzia, waalimu wa comb yako wa kutosha. kufika huku panda dom-moro/dar, then panda gari za dar-mbinga superfeo au saibaba watakushusha kigonsera stand utachukua bodaboda hadi shulen. karibu kaigo
 
Jamani nimepangiwa cbg kigonsera huko Ruvuma mi niko Dodoma naombeni msaada wenu kwa wanaifahamu hiyo shule kitaaluma,mazingira na anielekeze nitafika vp
Panda basi mpaka Songea, then utapanda lingine hadi kigonsera. Siku hizi kuna lami hadi Mbinga. Toka Songea hadi Kigonsera ni maximum of 1.5 hours. Usisahau mavazi ya kukukinga na baridi. Udongo ni mwekundu, wakazi wa kule wanaita NGUNJA. Mjini kwao kunaitwa Harare. Ukitoka Songea unafuata mtiririko ufuatao ki vijiji.... Ruhuwiko (Hapa kuna ST Joseph University, Njia panda ya Peramiho (Peramiho hospital), Njia panda ya Magagura (Kuelekea JKT Mlale), Kitai (Gereza la kitai, njia panda ya kuelekea Lituhi Nyasa), Mkako (Hapa kuna Likonde Seminary) then Kigonsera. Ni umbali wa kama 70kM toka Songea mjini. Wakazi wa hapo ni Wamatengo na mchanganyiko na wangoni....

Dispensari ya wakatoliki ipo maeneo ya shule, kuna kanisa la RC pia (sina uhakika na mengine na msikiti)

Jiangalie, kuna ngoma (ukimwi) ...

Nashukuru kwa msaada wenu lakini mbona bado mnanichanganya kuna anayesema nikitoka dar napanda basi la mbinga halafu nashuka kigonsera stand halafu mwingine anasema nipande basi la songea au kuna njia tofauti?
 
Dogo ngalikihinja atakuwa ameondoka muda mrefu huku, siku hiz kuna gari za dar -mbinga via kigonsera hakuna haja ya kulala songea mjini utaongeza gharama. vingine alivokuelekeza ni sahihi.
 
Dogo ngalikihinja atakuwa ameondoka muda mrefu huku, siku hiz kuna gari za dar -mbinga via kigonsera hakuna haja ya kulala songea mjini utaongeza gharama. vingine alivokuelekeza ni sahihi.

nashukuru kwa msaada wako mkuu!
 
Ni shule nzuri, hipo eneo zuri ambalo linamfanya mwanafunzi kuwa mdadisi katika kujifunza komaa kijana mambo yatakuwa vizuri.
 
Back
Top Bottom