Watanzania (viongozi na watawaliwa) kwa uzoefu na huenda kigenetic ni slow learners, kila kitu huwa tunafanya mwishoni kabisa na tunapigwa tu mara zote. Huwa tunasita na tunaogopa kila kitu hatimaye uoga unapopungua inakua too late na tushapoteza so hii itakujafanywa na generation ijayo kaka. Kwa sasa tuache tufe kwanza, watoto wa watoto wa 2000 watafanya tu haya. Yapo nje sana na ufahamu wetu wa kizazi hiki wa kukariri. Tazama mambo kama DECI, Mr Kuku, UPATU, Q-net nk, hata viongozi walipigwa (nao ni victims tu) ambao tungetegemea watuongoze kutuelimisha na kutahadharisha.
Sheria tu bado tunatumia na mkoloni mwingereza hatujaweza kutunga za kwetu miaka 60 baada ya uhuru, nchi zote zishahuisha katiba zao, sisi slow learners bado, kilimo chetu jembe la mkono, wakati watu wanafanya digital farming sasa, slow learners, kila mwaka tuna njaa chakula hakitoshi, slow learners, kila mwaka kuna mafuriko hadi ikulu, slow learners, kila mwaka watu wanakufa kwa kula mav na kupata kipindupindu, slow learners, shirika la ndege linapata hasara kila mwaka, slow learners tumezubaa tu na kusifia ndege, tunaagiza mafuta ya kula kwa matrilioni kila mwaka, slow learners, maprofesa wanakunywa mitishamba na mivuke kutibu covid, slow learners, maviongozi yana maphD lakini ni kama darasa la saba tu hoja zao, wanaojenga uchumi kwa kukopa na kuongeza makodi wakati uzalishaji ni uleule, slow learners, solution zetu kwa mambo mengi sana ni za kiroho yani ni uchawi na maombi, slow learners ndo maana mapsychopathy ya kidini yanaibuka na kuwalamba pesa na kutajirika wao tu na bado tu hatu-learn.
Hapa ukisema habari ya ardhi huria watasema wakenya wataiba ardhi yetu sijui wataiweka kwenye viroba? slow learners, uwekezaji watasema tunaibiwa wkt wanatuibia kwa kushirikiana nao, tamka diaspora watasema wanatishia usalama wkt sasa hivi hamna uraia pacha na usalama ni wa kufikirika tu! Anyway hamna diaspora atarisk nguvu zake kwa nchi unayoweza kuuwawa bila sababu na hamna hata uchunguzi kufanyika, yani yanaisha kiroho tu, utasikia mungu amlaze pema au mungu atamlipa NO!
Tuandaeni watoto kuwapa life skills wandugu tusirithishe hii slow learning kwa kizazi kijacho, angalau iishe kwetu.