Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ni tatizo la matamshi linalomfanya mtu asiwe na uwezo wa kutengeneza mpangilio wa moja kwa moja wa maneno na sauti anazotoa.
Watu wenye kigugumizi hufahamu maneno wanayotaka kutamka lakini hupatwa na ugumu katika kutengeneza mtitiriko wa matamshi hayo.
Changamoto hii inaweza kuambatana na tabia za kufumba macho, kukakamaa kwa misuli ya uso pamoja kutetemeka kwa midomo wakati wa kuzungumza. Pia, mambo yafuatayo huonekana-
Sababu
Sababu zinazofanya mtu apatwe na kigugumizi huwa hazipo wazi sana, lakini huhusianishwa na uwepo wa changamoto kwenye sehemu ya ubongo inayo ratibu lugha na matamshi, jini za urithi (genetics) pamoja na udumavu wa mtoto kwenye hatua za awali za ukuaji.
Aidha, mtu anaweza kupata kigugumizi baada ya kupitia kiharusi au ajali yoyote kubwa inayohusisha kichwa na ubongo.
Tiba
Tatizo hilo linalomfanya mhusika apunguze kujiamini, akwepe mazungumzo hasa yale yanayohusisha hadhara kubwa, ajihisi mnyonge pamoja na kudhihakiwa na watu wengine huwa halina tiba ya moja kwa moja isipokuwa kwa kila mtu, hutegemea umri wa mhusika, historia pamoja na matarajio yake.
Kwa watoto, kigugumizi mara nyingi huchukuliwa kama sehemu ya hatua ya ukuaji wao na huisha chenyewe baada ya kufikia umri wa walau miaka 6.
Hata hivyo, msaada wa matibabu hulenga kuongeza kujiamini kwa mhusika pamoja na kupunguza ukubwa wa tatizo na madhara yanayoambatana na uwepo wake.
Chanzo: Mayo Clinic/
National Institute on Deafness and Other Communication Disorders (NIDCD)

- Ugumu wa kuanzisha na kutamka maneno
- Kuvuta sana neno au sauti kwenye matamshi
- Kurudia kwa maneno
- Kuongeza maneno ya ziada mfano “um..” kati ya neno moja na lingine