Kaomba radhi i kupitia mtandao wa twitter akimjibu mdau mmoja aliemuhoji kuhusu kauli aliyowahi kuitoa kuwa atamuua mtu yoyote atakaeua twiga.
Tweet yake ya kuomba radhi hii hapa chini:
Niliongea kwa hasira. Nililipuka kutokana na uchungu dhidi ya wahalifu walioenda kuwinda nyara ya serikali ambayo ni alama ya Taifa bila hofu yoyote ile! Nilikosea na huwa najuta mpaka leo. Nilipaswa kuwa makini zaidi, kama Kiongozi ninayeamini utawala wa sheria/haki za binadamu.
Swali ni je, reaction ya watu kwa kauli ya Makamba pamoja na Mama kumuombea radhi Mzee Makamba kiana, ndio vimemfanya leo aone umuhimu wa kuomba radhi?