Kigwangala: Mzee Kikwete alisikia kilio cha Katiba Mpya, lakini walewale waliokuwa wanadai walikimbia

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
"Katibu tuliyonayo ni Bora sana. Hata kama ina mapungufu, basi madogo madogo sana. Na hayo yanaweza kusubiri kwa Kweli. Mzee Kikwete alisikia kilio cha wadai Katiba Mpya akaanzisha mchakato ili kuyarekebisha, kwa nia njema kabisa; lakini wale wale waliokuwa wanadai walikimbia!"- Kigwangala

1625479064804.png
 
Kutulia maanani maneno ya Kigwangala ni sawa na kujito ufahamu. Huyo kiumbe mithili yake ni wale dada poa wa barabarani. Ana uwezo wa kukwambia yeye ni bikra ili tu kukuridhisha tamaa zako.
 
Huyu Mh namfananisha na mzee alie kuwa na fursa akuzitumia sasa amebaki kupiga debe akumbukwe wakati ndio alishatemwa. Uwaziri
 
Kumbe anajua kuwa kuna kilio. Ila tumbo lake halimruhusu kufukiri vizuri. Watu hawajifunzi. Chawa waliumbuka baada ya mwendazake kwenda. Leo wanaanza tena uchawa!! Wengine ni mpaka damu iwatoke masikioni.
"Katibu tuliyonayo ni Bora sana. Hata kama ina mapungufu, basi madogo madogo sana. Na hayo yanaweza kusubiri kwa Kweli. Mzee Kikwete alisikia kilio cha wadai Katiba Mpya akaanzisha mchakato ili kuyarekebisha, kwa nia njema kabisa; lakini wale wale waliokuwa wanadai walikimbia!"- Kigwangala
 
Katiba pendekezwa Ni katiba ya 1977 iliyopakwa rangi tu..
 
Wanaodai katiba mpya sasa wamewahi kujiuliza nini kilisababisha mchakato wa mwanzo kukwama?
 
Ngoja ajaribu karata ya uteuzi na kufutiwa tuhuma za wizi zinazomkabiri.
 
"Katibu tuliyonayo ni Bora sana. Hata kama ina mapungufu, basi madogo madogo sana. Na hayo yanaweza kusubiri kwa Kweli. Mzee Kikwete alisikia kilio cha wadai Katiba Mpya akaanzisha mchakato ili kuyarekebisha, kwa nia njema kabisa; lakini wale wale waliokuwa wanadai walikimbia!"- Kigwangala

Naomba wanaccm mtusaidie kujibu hili swali, Ni yupi kati ya hawa wawili aliyekimbia mchakato wa katiba mpya;
1. Aliyebadilisha maoni ya wananchi (yaliyokusanywa na Tume ya warioba) kwa kuyatupa kapuni na kuleta ya kwake (waliyoyapa jina katiba pendekezwa), au
2. Aliyekataa kujadili maoni ambayo sio ya wananchi?
 
Mchakato wa kwanza ulikwama kwa sababu ya kilicholetwa mezani na akina Warioba sio kilichokuwa kinakwenda kupitishwa
 
"Katibu tuliyonayo ni Bora sana. Hata kama ina mapungufu, basi madogo madogo sana. Na hayo yanaweza kusubiri kwa Kweli. Mzee Kikwete alisikia kilio cha wadai Katiba Mpya akaanzisha mchakato ili kuyarekebisha, kwa nia njema kabisa; lakini wale wale waliokuwa wanadai walikimbia!"- Kigwangala

Jinga hili
 
Wanaodai katiba mpya sasa wamewahi kujiuliza nini kilisababisha mchakato wa mwanzo kukwama?
Point muhimu Sana ,hii kudai katiba mpya muhimu tukaanzia pale tulipoishia na kujua sababu ya kusitisha katiba kwa kipindi kile ,na sababu ya kuipiga chini katiba ya warioba na kuleta ya ambayo haina maana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom