Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Namshanga sana Dkt. Kigwangalla kumshambulia Dkt.Bashiru juu ya uanachama wake. Kama mwana chama wa CCM sijapendezwa na kauli yake kwa sababu CCM kinaamini kila mwanachama ni sawa na mwingine bila kujalisha ukongwe wake ndani ya Chama.
Bila kujalisha alikuwa nani kabla ya kuwa mwanaCCM ,Dkt.Bashiru alikuwa na haki zote za mwanachama baada ya kuwa mwanachama wa CCM hivyo ninaamini alikuwa ana haki zote za kuwa KM wa CCM kama wanachama wa vyama vingine.
Pia, ukisoma kanuni na katiba ya CCM juu ya kukoma uanachama wa mwanachama unaona uanachama unaweza kukoma kwa mwanachama kujiunga na chama kingine. Ninaamini kipengele hiki kipo kwa kila chama.
Kwa mantiki hii Dkt.Bashiru hakuwa katibu mkuu wa CCM kwa kujiteua na mchakato wake ulipitia taratibu zote kama kupitishwa na NEC na CC, Je ni kweli NEC na CC ilibariki mwana CUF kuwa katibu mkuu?
Pia, tukumbuke kabla ya kuwa Katibu mkuu alikuwa mwenyekiti wa kamati iliyoundwa Mali za chama na kamati ile ilipata baraka za kamati kuu. Je, bado tunaendelea mashaka uanachama wa Bashiru ?
Zaidi ,uanachama sio kadi ni imani na Dkt.Bashiru kaiishi imani ya chama na hatupaswi kuwa na mashaka na uanachama wake kwa kuwa ni mtiifu kwa Chama.
Maneno ya Kigwangalla sio tu yakupotosha ni kubomoa