Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 katika Jimbo la Nzega Vijijini umeacha gumzo zito, baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Hamisi Kigwangalla, kudaiwa kuangushwa kwa hila, hujuma na mchezo mchafu wa kisiasa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya vikao vya wajumbe, mchakato huo uligubikwa na vitendo vinavyodaiwa kuwa vya kupanga matokeo kwa makusudi ili kumng’oa Dkt. Kigwangalla, ambaye alikuwa akiwania ridhaa ya kurejea bungeni kupitia tiketi ya CCM. Wajumbe kadhaa wameeleza kuwa kura zake “zilipigwa chooni” – ishara ya wazi kuwa hakuheshimiwa wala kupewa nafasi ya haki kama mwanachama na kada mwandamizi wa chama hicho.