Kigwangalla na Lusinde mnahoji uanachama wa Dkt. Bashiru, mbona hamkuhoji alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM?

Kigwangalla na Lusinde mnahoji uanachama wa Dkt. Bashiru, mbona hamkuhoji alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM?

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
CCM oyee!

Zidumu fikra za mwenyekiti Magufuli
Bashiru Ally aliteuliwa na mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli, hamkupiga ktk kikao chochote zaidi ya kumpongeza huku KIgwangalah ukijua kuwa Bashiru ni mwanachama wa CUF.

Wapinzani waliteuliwa na kupewa nyadhifa serikalini huku mkijua serikali iliyopo sio ya umoja wa kitaifa lakini hamkupinga zaidi ya kumpongeza mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli.

Wapinzani walinunuliwa na kupitishwa kugombea udiwani na ubunge kwa tiketi ya CCM bila kupewa au kusalimisha kadi za uanachama wao huko walikotoka hamkupinga wala kuhoji zaidi ya kumshangilia mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli.

Huo ni inafiki wa kisiasa.

plustvtz_1669209558452135.jpg
plustvtz_1669236001301235.jpg
 
Ng'ombe zaidi ya 5,000 walivamia vichwani mwao na kunywa akili zao, sasa Ng'ombe mmoja anakunywa akili 45 kwa siku na hao wawili wana akili mbili. Lazima kuwe na uhaba.
 
Wakitaka hivyo wawatimue wote waliotoka upinzani na kupewa ukuu wa wilaya na ubunge.

Patamu hapo na sijui nani ataanza
Lakini pia kuanza kuhoji nani anastahili kwenye chama ndo yale yale mwalim Nyerere alisema mkiwamaliza hao mtaanza kujiangalie na nyie nani hafai
Shida ya hicho chama ukiwa ndani hupaswi kuuongea ukweli
 
Hatujui nani walihoji uanachama wa Bashiru lakini ni dhahiri wapo waliofanya hivyo. Haya yalithibitishwa na mwenyewe Magufuli aliposema chamani aliambiwa unamleta Bashiru ni CUF huyu. Kisha akasema CUF wa namna hii ndiwo anaowataka.
 
Shida ya chama dola hawataki kuhojiwa na Wananchi, ebu waza kauli ya Balozi ina ubaya gani? Tukitaka kufika mbele lazima tufanye mageuzi makubwa sana. Tunahitaji katiba mpya na kubadilisha mfumo wote wa kuendesha nchi.
 
Thubutu,wahoji hawajipendi

Asilimia kubwa ya watanzania ni wanafki wakiongozwa na hao wanasiasa

Ova
 
hao wote ni waganga njaa na ni wa kupuuzwa tu hawana lolote la maana.kibajaji anaishi kwa uchawa kwake ni kawaida tu kutoa kauli kama hii lkn wakati ule wa chuma wote walifyata midono halafu leo wanatafuta political mileage.

kigwa elimu yake haijamsaidia chochote.kama yeye ni Dr na ameshindwa kuitumia elimu ili kujipatia ridhiki unategemea nn!hao ndo wanaowadanganya vijana wajiajiri wakati wao wameshindwa kujiajiri na badala yake wamejibanza kwenye ajira za kisiasa.apractice elimu yake tumwone.
 
Hii tabia ya unafiki nafiki inaitafuna sana hii nchi, watu hawajikiti kwenye fact baadala yake wako kwenye utetezi wa upande wanapopatia ugali... tunadumaza bongo zetu na aina hii ya viongozi wanaliangamiza Taifa.
 
Hatujui nani walihoji uanachama wa Bashiru lakini ni dhahiri wapo waliofanya hivyo. Haya yalithibitishwa na mwenyewe Magufuli aliposema chamani aliambiwa unamleta Bashiru ni CUF huyu. Kisha akasema CUF wa namna hii ndiwo anaowataka.
Kama Magufuli alijibu hivyo ni Wazi Walimkubali VIPI TENA leo WANAHOJI AU Ubongo wao umejaa Maji?
 
Wajinga tu hao. Leo ndo wanahoji uanachama wa Bashiru.
Badala ya kujibu hoja za Msingi, wao wanakwepa wanakimbikia kuhoji uanachama. Ovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom