Kigwangalla usokolokwinyo huu atauacha lini?

Kigwangalla usokolokwinyo huu atauacha lini?

Viongozi wengi ni opportunistic, anaenda na upepo wa mama........mama ghafla akiondoka aje mwingine aseme anataka katiba utaona jitu kama HK litakavyogeuka kama poyoyo. Wanasiasa wetu ni wanafiki sana......baada ya kifo cha jeipiemu ni uthibitisho tosha wa unafiki wao
 
Usokolo kwinyo
mjlol.png
 
..Pia ni mwizi wa kazi za watu "Plagiarism" maana hicho alichoandika hapoo ni nukuu ya maneno aliyosema Palamaganda kabudi...sio maneno yake hasa na kwa kuwa haja shukuru "acknowledge" chanzo basi ni wizi....Japo wote wawili kwa maneno hayo ni KUTU YA NG'OMBE (kwa sauti ya Mzee Mwai Kibaki wa Kenya)
 
Dk Kigwangalla ana sifa zote za mtu aitwaye HASIDI. Hasidi ana pande mbili:- upande ni mtu mwema na upande mwingine mnafiki. HK anacheza na vitu 2:- bosi wake na nyakati. Siyo wa kuamini tena huyu Ni kisokolokwinyo aliyeenda shule.

Akiwa waziri wa afya aliunga mkono wazo la jpm la watu kujifukiza. Akalipigia chapuo sana na akawa anarusha clip na picha akionesha anavyojifukiza. (Hapa HK alikuwa analinda ugali, hivyo akawa anajipendekeza kwa kiwango cha sgr kwa bosi wake).

Lkn siku chache tu baada ya kifo cha Magufuli alianza kupinga kujifukiza. (Hapa alishaona Magufuli hana ishu tena. Wa nini? Hatomsaidia kwa lolote. Nyakati za Magufuli kuwa bosi zimepita).

Na sasa ameanza kujipendekeza kwa mama Samia (Soma maoni yake hapa chini juu ya katiba mpya). Nadhani anatafuta uwaziri. Je, anaaminika tena hasidi huyu?? Anaaminika tena kisokolokwinyo huyu?

Mbona Dr. Kigwangallah yuko sahihi.....mwenye matatizo hapa ni wewe na wale wenye mtizamo kama wako. Hapa tatizo la Kigwangallah ni nini, ebu tueleze?
 
alichoandika hapoo ni nukuu ya maneno aliyosema Palamaganda kabudi...
Huyu Kabudi naye kwa kweli ndiyo wale wale tu. Alikuwa kwa tume ya jaji Warioba ya katiba mpya. Lkn anavyoongea utadhani kashuka toka sayari ya Pluto.

Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
 
Usilokwinyo..Daaah! Kiswahili hadi raha. Huyu Jamaa uwa Namwona kama Mshamba fulani. "Opportunist"
 
Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
Wasomi wa nchi hii wakiingia kwenye siasa hawafikiri kwa kutumia vichwa tena...hufikiri kwa kutumia tumbo....kumbuka Mwakyembe alikana andiko lake la PhD juu ya serikali Tatu! umemsikia Issa Shivji....!
 
Aje Emmaus Ubungo afanyiwe maombi. Pengine ana Pepo la unafiki. Tooooka pepoooo.... .
 
Huyu Kabudi naye kwa kweli ndiyo wale wale tu. Alikuwa kwa tume ya jaji Warioba ya katiba mpya. Lkn anavyoongea utadhani kashuka toka sayari ya Pluto.

Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
Ni asili na mifumo hata wewe ukiwa mwanasiasa utakuwa hivyo hivyo

Usifikiri kibinadamu una utofati nao sana
 
Back
Top Bottom