Kigwangalla usokolokwinyo huu atauacha lini?

Viongozi wengi ni opportunistic, anaenda na upepo wa mama........mama ghafla akiondoka aje mwingine aseme anataka katiba utaona jitu kama HK litakavyogeuka kama poyoyo. Wanasiasa wetu ni wanafiki sana......baada ya kifo cha jeipiemu ni uthibitisho tosha wa unafiki wao
 
..Pia ni mwizi wa kazi za watu "Plagiarism" maana hicho alichoandika hapoo ni nukuu ya maneno aliyosema Palamaganda kabudi...sio maneno yake hasa na kwa kuwa haja shukuru "acknowledge" chanzo basi ni wizi....Japo wote wawili kwa maneno hayo ni KUTU YA NG'OMBE (kwa sauti ya Mzee Mwai Kibaki wa Kenya)
 
Mbona Dr. Kigwangallah yuko sahihi.....mwenye matatizo hapa ni wewe na wale wenye mtizamo kama wako. Hapa tatizo la Kigwangallah ni nini, ebu tueleze?
 
alichoandika hapoo ni nukuu ya maneno aliyosema Palamaganda kabudi...
Huyu Kabudi naye kwa kweli ndiyo wale wale tu. Alikuwa kwa tume ya jaji Warioba ya katiba mpya. Lkn anavyoongea utadhani kashuka toka sayari ya Pluto.

Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
 
Usilokwinyo..Daaah! Kiswahili hadi raha. Huyu Jamaa uwa Namwona kama Mshamba fulani. "Opportunist"
 
Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
Wasomi wa nchi hii wakiingia kwenye siasa hawafikiri kwa kutumia vichwa tena...hufikiri kwa kutumia tumbo....kumbuka Mwakyembe alikana andiko lake la PhD juu ya serikali Tatu! umemsikia Issa Shivji....!
 
Aje Emmaus Ubungo afanyiwe maombi. Pengine ana Pepo la unafiki. Tooooka pepoooo.... .
 
Huyu Kabudi naye kwa kweli ndiyo wale wale tu. Alikuwa kwa tume ya jaji Warioba ya katiba mpya. Lkn anavyoongea utadhani kashuka toka sayari ya Pluto.

Sijui Kuna shida gani nchi hii? Kwann watu wanakuwa wanafiki hivi??
Ni asili na mifumo hata wewe ukiwa mwanasiasa utakuwa hivyo hivyo

Usifikiri kibinadamu una utofati nao sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ