KIGWANGALLA: Wawekezaji wa Vitalu wanahonga sana pesa, wapo tayari KUUA wapate wanachotaka, ukikataa wanakutegea mtego wa Rushwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Your browser is not able to display this video.
Mwanasiasa Dkt Hamis Kigwangalla amezunguzia Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo amewahi kuiongoza akisema kuwa ukiwa Waziri wa hapo utahongwa sana hasa kutoka kwa wawekezaji wa vitalu.

“Wawekezaji hasa wa vitalu wanapenda kuwa na maeneo makubwa, wale wa picha siyo sana, watu wa vitalu hawawezi kuacha wanachofanya kwa njia yoyote ile mpaka wapate wanachokitaka.

“Kama anataka kitalu fulani, atahonga, atafanya chochote, anaweza kuua mtu au kuua wananchi ilia apate eneo, wana tamaa na kiu ya kupata vile vitalu

“Ukiwa Waziri pale utahongwa sana pesa, usipotolewa kwa kuwanyanyasa wananchi basi utafukuzwa kwa rushwa au wawezaji wenyewe wakuwekee mtego au mwenyewe utashindwa kazi, kuna mambo mengi yamezunguka ile Wizara…

“Baada ya mimi kuteuliwa, nilifuatilia na nikajiweka mambo ya kuzingatia, kwanza kutochukua pesa, pili kuwa muwazi, tatu kufanya maamuzi ya pamoja ya idara zote zilizo chini ya Wizara, sikutaka kujifungia kufanya maamuzi peke yangu,” - Hamis Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini.

Source: EFM
 
Hii ina maana gani kwa swala la Ngorongoro??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…