Kigwangwala: Mbowe asikubali kushindwa na Lissu atakuwa fala kumuachia chama

Ukiona mpaka mwenyekiti anatupiwa dongo zito hivyo na wafuasi wa chama tawala, basi jua amepuyanga sana kwa uamuzi wake huo.

^Ndugu zangu, nimewasikiliza vizuri. Nipeni saa 48. Leo ni Jumatano. Kesho na Ijumaa. Jumamosi saa tano asubuhi, nitatangaza msimamo wangu hapa hapa. Nikiona chama CHANGU kinaenda kuzamishwa, mimi kamanda NARUDI mzigoni.^
 
Kwani hiki chama ni kampuni binafsi au taasisi ya umma/wanachama?

Huyo kigwangalla ni mpuuzi sana, ni vyema Mbowe angeamua tu kuachia madaraka kwa hiari Ili kulinda heshima na Legacy yake.

Kufikia hatua ya kuanza kutetewa na wapinzani wako eti chama umekitoa mbali ni hatua za mwisho za kushindwa kuwa kiongozi mzuri.

Unapoanzisha chama Cha siasa na kupata uungwaji wa watu haimaanishi kuwa wewe unawamiliki na kuamua lolote dhidi Yao.

Jambo lolote linapokuwa la watu na dira ya watu basi siyo mtaji wa mtu mmoja bali ni kwa maslahi ya umma.

Again Mbowe kubali kuachia kijiti wafanye na wengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…