carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, amewawashia ‘taa nyekundu’ watumishi wa umma wanaojiona wako juu ya chama hicho tawala, akisema hakitasita kuchukua hatua dhidi yao.
Kihongosi ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Oktoba 18, 2026, akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani, akisisitiza kuwa nidhamu na uwajibikaji ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
Amesema CCM ndiyo iliyounda Serikali iliyopo madarakani, hivyo hakuna mtumishi wa umma anayepaswa kujiona mkubwa kuliko chama hicho: “Ndio chama kilichounda Serikali. Maana yake Serikali iliyoko madarakani imewekwa na Chama cha Mapinduzi, kwa hiyo asitokee mtumishi yeyote wa umma akajiona yuko mkubwa kuliko chama. Chama hakitavumilia hilo jambo.”
Kauli hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlawa, kudai baadhi ya watendaji wa vijiji hawataki kuwajibika kwa chama hicho.
Akijibu hoja hiyo, Kihongosi amesema chama kitashughulikia watumishi wazembe na kusisitiza kuwa kitakagua miradi ya maendeleo kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa, bila rushwa wala ucheleweshaji usio wa lazima.
Amesema viongozi wa Serikali kuanzia ngazi za mikoa na wilaya wanapaswa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma na miradi inakamilika kwa wakati.
Chanzo :Mwananchi official