Kihongosi: CCM Haitishwi na ninadhibitisha hapa chama hiki hakitatoka madarakani

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, ametoa msimamo mkali dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani, akisisitiza kuwa CCM haitishwi, haitaondoka madarakani kwa matamanio au maneno ya kisiasa, na ipo tayari kushindana kupitia sanduku la kura kulingana na kazi kubwa za maendeleo zilizofanyika.

Kihongosi ameyasema hayo leo, Jumamosi Oktoba 17, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani

"Leo ninadhibitisha hapa chama hiki hakitatoka madarakani. Kazi iliyofanyika ni kubwa kitaendelea kuongoza taifa hili. Chagua maendeleo sio maneno, na nchi yetu ina mifumo ya kidemokrasia, twende kwenye sanduku la kura tukapigiane kura watu waamue. Sio kusema CCM iondoke madarakani. Hiyo biashara haipo." Amesema Kihongosi.

Kihongosi amewasihi Watanzania kulinda amani na ardhi yao, akibainisha kuwa hakuna mgeni au mzungu kutoka duniani atakayeipenda na kuilinda Tanzania kuliko Watanzania wenyewe.

“Hiki chama hakitishwi... Tuna mambo mengi ya kusimamia ndani ya nchi hii: maendeleo ya vijana wetu, maendeleo ya kina mama, maendeleo ya wazee. Tunawaza kujenga hospitali, kuboresha huduma za afya, miundombinu ya barabara na reli, tunawaza uchumi upande. Kuna mtu anawaza kuchoma, haitawezekana na haitakubalika”, ameeleza.

Ccm haitishwi wakati mnambeleko zote za dola lakini bado mnachemshwa na CHADEMA vibaya sana
 
Kuondoka itaondoka Brother! Kunywa supu nyama ziko chini!
Hata utawala wa Hitler ulifika mwisho!
 
Back
Top Bottom