Kihongosi: CCM ndio muasisi wa katiba mpya, mchakato utapatika kabla 2030

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya nchini ni ajenda yake ya msingi na utatekelezwa kama ulivyohaidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025–2030.

Akizungumza kwenye mahojiano ya mojakwa moja na Clouds Digital leo 19/08/2026, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Itikadi, Uenezi na Mafunzo), Kenani Kihongosi, ameeleza kuwa CCM ndiyo muasisi wa ajenda ya Katiba Mpya na kamwe haijawahi kuogopa wala kukimbia mchakato huo kwa kuwa ni jambo lenye maslahi mapana kwa taifa.

Soma pia: Kihongosi: Katiba mpya ni ajenda ya CCM na tuwahakikishie Watanzania kabla ya 2030 tutakuwa na katiba mpya

Kihongosi amebainisha kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa Katiba Mpya ni kipao mbele na Serikali itakutana na wadau wote ili kuhakikisha inapatikana. Ameongeza kuwa Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Serikali ya CCM ndio walioanzisha mchakato huo, huku Dkt. Samia akiwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba mwaka 2014.

Aidha, Kihongosi ameeleza kuwa mchakato huo ulipata mikwamo huko nyuma kutokana na hatua ya vyama vya upinzani vilivyounda umoja wa UKAWA kususia Bunge la Katiba mwaka 2014 wakati mchakato ukiwa katika hatua za mwisho za kupigiwa kura.

Kihongosi amesema, "Chama Cha Mapinduzi ni waasisi wa jambo hili na tunalitaka, sio kwamba hatulitaki na wala hatuliogopi kwa sababu ni jambo jema... Katiba Mpya itapatikana."

Sasa huyu chawa ndio anataka mdahalo na heche mbona anajitafutia aibu ya karne
 
Anasema hivyo kwa sababu ameshiba. Akitolewa hapo anaanza kulia huruma kama Tulia.
 
Back
Top Bottom