"Chama hiki ni chama cha watanzania wote, hiki ndo chama pekee kisicho na ubaguzi, hiki ndo chama pekee kinachojali vyama vyote, hiki ndo chama pekee kinachojali utu wa watanzania, chama cha mapinduzi kwa lugha nyepesi tunaita hii ni full package imejaa na imetimia, hiki ndo chama imara. Jambo lingine chama hiki hakitingishiki, hakitikiswi, hakitayumba katika msimamo wa kupeleka maendeleo kwa watu wake"-
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Ikungi mkoani Singida, katika mkutano uliofanyika Kata ya Puma leo Januari 22, 2026.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Ikungi mkoani Singida, katika mkutano uliofanyika Kata ya Puma leo Januari 22, 2026.