Kihongosi: CCM tunaamini katika maridhiano, tunatoa rai kwa makundi yote kushiriki

Joined
May 2, 2026
Posts
64
Reaction score
55
KIHONGOSI:CCM TUNAAMINI KATIKA MARIDHIANO,TUNATOA RAI KWA MAKUNDI YOTE KUSHIRIKI

Katibu wa Idikadi,Uenezi,Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kenan Kihongosi amesema Chama hicho kinaamini katika maridhiano kwani maridhiano yakipewa nafasi migogoro inapungua.

Kihongosi ameyasema hayo leo Mei 4,2026 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari ambapo amesema sio mara ya kwanza katika nchi kufanyika maridhiano.

“CCM kama chama tunaamini katika maridhiano na maridhiano haya si ya kwanza kufanyika au kutokea katika nchi yetu.Katika nyakati ambapo kelele au tofauti ya kisiasa katika jamii au itikadi zinapoongezeka jambo moja linabaki kuwa la msingi kuliko yote hatma ya Taifa haiwezi kujengwa juu ya misimamo mikali bali juu ya uwezo wa kukaa pamoja na kusikilizana

“Chama Cha Mapinduzi kinaamini pale mazungumzo yanapopewa nafasi migogoro inapungua ,taasisi zinaimarika na maendeleo yanapata mizizi imara hasa katika kuwatumikia wananchi,”amesema.

Amefafanua kwa muktadha huu wanatoa mwito wa kushirikisha makundi yote yakiwemo vyama vya siasa ,viongozi wa dini ,asasi za kiraia ,vyama vya wafanyakazi,sekta binafsi ,viongozi wa kimila ,wananchi na wadau wa maendeleo katika uwepo wa maridhiano.

“Kwasababu watu wanaamini kwamba maridhiano ni baina ya vyama vya siasa hapana bali ni mambo yanahitajika kuzungumzwa kwa upana wake na nchi yetu inavyama zaidi ya 18 maana yake vyama hivyo vinauwezo wa kushiriki kuridhiana katika maeneo ambayo tunaona yanamsingi huo

“Tunasema hivyo tukitambua sio wadau wa pembeni niliowaorodhedha bali ni wadau kwa maslahi ya Taifa wanapoamua kuweka maslahi ya nchi mbele badala ya maslahi binafsi wanakuwa tu si sehemu ya suluhisho bali ni mustakabali wa kudumu kwa amani ya taifa letu.”

Kihongosi amesema pia kama ilivyo falsafa ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya 4R ambayo ni maridhiano, Ustahimilivu, mageuzi na ujenzi upya imefungua dirisha la historia ambalo halipaswi kupuuzwa.
 
Je katika kutekana, kuuwana na kupeana kesi feki nako mnaamini?
 
Polepole aliwaambia mfanye maridhiano kabla ya uchaguzi mkakaza shingo Halafu sasa ndio mnayataka punguwani waheedi… achani kuwataka watanzania kwa kauli za jumla jumla zilizokosa tafakuli tunduizi…
 
Back
Top Bottom