Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi amewataka Watanzania kutokubali kauli zinazowahamasisha kuchukia vyombo vya ulinzi na usalama, akisisitiza umuhimu wa kuwaheshimu na kuwapa moyo askari wanaolinda usalama wa taifa.
Kihongosi amesema askari huendelea kufanya doria na kulinda wananchi wakati wengine wakiwa kwenye shughuli zao za kila siku au wakilala. Amewataka wananchi kutambua mchango wa askari na kuwapa ushirikiano katika kulinda amani na usalama wa nchi.
Akizungumzia kauli za kuwachukia askari, Kihongosi amemjibu mtu anayehusishwa na kauli hizo kwa kusema: “Wewe bwana umechanganyikiwa, tuondolee ujinga hapa!” Aidha, amewataka wananchi kuungana katika kulinda taifa, akisisitiza kuwa jukumu la ulinzi wa taifa ni la wananchi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.