Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amewataka Watanzania kuamini katika nguvu ya mazungumzo kama njia pekee ya kuleta mageuzi ya kweli na maendeleo nchini, badala ya kukimbilia maandamano ya barabarani au vurugu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 4, 2026, Kihongosi amesisitiza kuwa mageuzi yenye tija hayazaliwi kupitia majukwaa ya lawama au shinikizo, bali yanapaswa kupikwa kwenye meza ambapo hoja mbalimbali hukutana na kuchambuliwa kwa kina ili kufikia mwafaka wa kitaifa.
"Mageuzi ya kweli hayazaliwi barabarani pekee, wala kwenye majukwaa ya kisiasa au majukwaa ya lawama, bali katika meza ya mazungumzo ambako hoja hukutana, tofauti huchambuliwa na mwafaka hupatikana,"-Amesema Kihongosi.