Kihongosi na CCM achaneni kuwasingizia Chadema, angalieni muungano unavunjika. Sikia maneno ya sheikh

Kihongosi na CCM achaneni kuwasingizia Chadema, angalieni muungano unavunjika. Sikia maneno ya sheikh

Nyerere alikuwa mamluki wa qeen mwenye kununa na anune

Uhuru una gharama Iweje yeye aupate mezani.!?

Hicho kiwilaya cha zanzibar kilipata uhuru kwa mtutu Eti yeye bahari ya Tz kapewa mezani.! Upuuzi

Mimi Abeid karume nina hakika alikuwa radhi kuunga Zanzibar na Tanganyika mazima

Nasema hivyo kwakuwa nawajua watu wa pwani hawana uroho

Ila huyu master mind wa butihama nina Hakika ndiye aliyeweka vile vipengele vya muungano Mnafki sana yule mzee

Hilo mbona alilisema mwenyewe ? Karume alikuwa tayari kuua Zanzibar tuwe nchi moja.

Nyerere akakataa, akalazimisha hiki kituko.

Zanzibar ilipaswa kubaki kivyake na Tanganyika kivyake kama Tanzania na Malawi au na Burundi.

Unaunganishaje nchi na kawilaya kamoja ???

That was a foolish move by Nyerere
 
Watanganyika endeleeni kupaza Sauti ya Utaifa ya Tanganyika.

Kadri Wazanzibari wanavyojibu ndio mpasuko ndani ya Jamii unaongezeka, sikiliza kwa makini huyu Sheikh anayozungumza alafu useme kwa nini kusiwepo na Serikali ya Tanganyika.

CCM mjibuni huyu Sheikh.

View attachment 3607267
Tanganyika ikitunga sheria kandamizi kuwapendelea watanganyika sawa au kuliko za kwao, wao ndiyo watalia na kusaga meno,utasikia mayowe, tunaonewaaaa tunaonewaaaa.

Akitokea jasiri kama Tuntemeke Sanga, Kashemeza Kabuye, Njelu Kasaka nk utaona mziki wake mabaguzi mazaznzibar yatakavyo lalamika.

Ubaya tumeingiza mkia makalioni na kuufyata kimya.
 
Back
Top Bottom