#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana CCM hao?

---
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la ya Covid-19, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.

"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan "

"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali."

"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza"

"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja"

"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu"

Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
Huyu nae ni muda utaongea . Kwenye kesi ya sabaya mashahidi wanamtaja sana kama mfadhili wa sabaya .siyo mkuu wa polisI upelelezi wilaya na diwani ccm aliye vamiwa .lazima ataitwa nayeye
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana CCM hao?

---
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la ya Covid-19, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.

"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan "

"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali."

"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza"

"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja"

"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu"

Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
Analinda tonge lake huyo hana jipya!
 
Huyu Kihongosi mbona anatumia nguvu sana kupambana na wenzake!! Ila aweke akiba ya maneno maana hizi siasa Zina kurasa nyingi sana.
Anatakiwa awajibu kina zito na kina heche.
Umemshauri vizuri, asome wenzake na alama za nyakati akumbuke walikuwepo watu kabla yake.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
ka polepole katakuja kufukuzwa chama kakoswe pa kujishikiza hizi takataka sijui JPM aliziokotea wapi
Umehitimu 2016, ajira huna na unategemea kuajiriwa na serikali iliyowahi kuwa na takataka aina ya polepole😂.

Kati yako na polepole,ni nani anaeishi Tz kama takataka?
 
Umehitimu 2016, ajira huna na unategemea kuajiriwa na serikali iliyowahi kuwa na takataka aina ya polepole😂.

Kati yako na polepole,ni nani anaeishi Tz kama takataka?
wewe na pole pole mnaishi kama takataka😀😀 na wewe pia ni takataka
 
Kenan awe na maneno ya akiba, siasa ni mchezo wa ajabu sana,leo unang'ata,kesho unang'atwa na kutafunwa!

Polepole kwa kazi aliyokua nayo,anajua uhuni wote wa Chama,so kijana,Kenan awe na maneno ya akiba!
Zam kwa Sam wewe kenge,afu Kenan ni mkongwe kwenye siasa kuliko Polepole wenu
 
Kihongosi aache ujinga bana,si kila mtu sababu yupo CCM basi aseme yale yanayomfurahisha kiongozi wao, kama mwenyekiti wake anasema kuchanja ni hiari na Polepole anasema hachanjwi tatizo lipo wapi? katibu wa jumuia ya vijana wa CCM ndio kawa msemaji wa CCM? nchi hii kila mtu yupo huru kusema lolote maadamu havunji sheria, sasa kwa kifungu kipi cha sheria au katiba kinasema ukisema tofauti na raisi ni kosa, huyu dogo aache kutoa matamko na kiherehere chake cha kujikomba hakitamsaidia kitu.
Basi wewe ni mgeni na ccm,uvccm huwa ni genge au wing ya kutisha watu uwe ndani ya chama au nje ilimradi watalinda maslahi si TU ya mwenyekiti bali na ya chama kwa namna yoyote.

Wanaotekaga na kuzingua watu ni akina nani? Kwa hiyo kama huwajui maccm kaa kimya yasije yakakufika
 
Ni kweli serikali imeshasema suala la chanjo ni hiari,hivyo anachofanya mh.Polepole siyo sawa kuwachanganya wananchi kwani yeye siyo mtaalam wa afya.ilikuwa ni lazima kuleta chanjo kwa makundi ambayo huwezi kuwanyima fursa hiyo kama mabalozi,taasisi za kimataifa, watu wa mataifa ya nje ambao nchi zao zimeshaweka sharti la lazima,pia wananchi ambao wanasafiri nje iwe kibiashara ama shughuli nyingine(kwani mataifa mengi swala hili ni lazima) pia wazee na wengine wenye uhitaji.Ukiwa kiongozi wa nchi lazima uangalie makundi yote.Yeye na wengine kama hawataki basi wakae tu kimya na maisha ya endelee,kama Mh.Mbunge kuna kero nyingi za kimaendeleo zinazokabili wananchi ndio ni vyema aishauri serikali.
Tena na gwajima kwa kujifanya anahubiri wakati anatekeleza maswala ya kisiasa kinafiki kwa kutumia jukwaa la dini,watch out
 
Pesa zake zipo Tanzania shughuli zake zipo Tanzania kwenda nje hawezi hajachanja.Katiba yetu mbovu imempa madaraka makubwa mtu mmoja. Hivi wakimfanyia figisu kanisa lake likafungwa,akaunti zake zikawafreezed kupisha uchunguzi utasema Gwajima Hana Njaa?

Kama Kweli Gwajima mwamba kwanini kwenye kauli zake anamponda waziri lkn hapohapo anasema anamuunga Mkono Rais hampingi?
Anachotakiwa Gwajima Ni kutokujisahau na kuvuka Mstari.
Mbona Magu tuu alimpa msukosuka akaufyata unadhani mama anashindwa? Si anamsitahi tuu ila asivuke mipaka.

Sakata la Mbowe limewapa picha kwamba Maza sio wa kuchezewa
 
Huyo jamaa naye zoba tu.

Mzee Warioba amejitokeza na kuweka misimamo Yake kuhusu Katiba mpya ambayo inakinzana na ya huyo Mama yake ila hajaibuka na tamko lolote.

Kutaka watu wote wakubaliane na mama yake hata Kwa mambo ya hiari ni upumbavu.
Acha upumbavu wewe,Wapi mh Rais kasema anapinga Katiba?

Afu ushasema Mzee warioba ,yeye ni status tofauti kabisa na huyo mpuuzi wako.

Ni hivi enzi za vietell zimepita aufyate.
 
Back
Top Bottom