Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia kwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, kimeishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwenye mafuta. Hatua hiyo inalenga kupunguza gharama za nishati hiyo nchini ili kumpunguzia mwananchi mzigo wa maisha
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Chama kinachoisimamia serikali, tumeishauri Serikali kuona ni kwa namna gani inaweza kuangalia mpango wa kutoa ruzuku ili kuweza kidogo kupunguza gharama za mafuta kama ambavyo Rais Samia alifanya hivyo katika kipindi cha mwaka 2022.."
Hayo yameelezwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kihongosi wakati wa Mkutano wake na Vyombo mbalimbali vya habari, leo tarehe 7 Aprili 2026, Jijini Dodoma.