Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi ametoa onyo kali kwa watu wanaochochea vurugu nchini, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia vitendo vinavyohatarisha amani ya taifa, huku akiwataka wananchi kuwa macho dhidi ya ushawishi wa watu wenye ajenda binafsi.
Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani Muleba mkoani Kagera, amesema kuna baadhi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaojaribu kupotosha wananchi na kuhamasisha machafuko, jambo alilosema halipaswi kupewa nafasi. Aliongeza kuwa Watanzania wanapaswa kuthamini maisha yao na kulinda amani waliyonayo, kwani mataifa mengi yanahangaika kuitafuta bila mafanikio.
Aidha, amesema mara nyingi wanaochochea vurugu ni watu wazima wanaowatumia vijana kutekeleza matendo hayo, na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao bila kusita. Amewataka wananchi wa Muleba kulinda ardhi yao kwa wivu mkubwa na kutojiingiza katika makundi au harakati zenye malengo ya kuvuruga utulivu wa nchi.
