McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
VIDEO:
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amewakumbusha viongozi wa serikali kuwa CCM ndicho kilichounda serikali na hivyo kiko juu yao na kitaendelea kuisimamia kikamilifu.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Kihongosi amesema viongozi wote wa serikali wanapaswa kutambua kuwa chama kitaendelea kuchapa kazi na hakitasita kushughulika na wazembe katika ngazi zote.
Zaidi Soma: Kihongosi: Heche Anajua Muenezi wa CCM Sio Size Yake, hasa Katika Mdahalo. Aje na Lema, Boniyai na Sugu
"Na viongozi wa serikali lazima wajue chama ni kikubwa kuliko serikali. Lazima wafahamu chama ndio kimeunda nini serikali. Lazima tuisimamie kikamilifu. Kwa hiyo ndugu zangu wa Ilala, chama chenu kitaendelea kuchapa kazi," amesema Kihongosi.
Kihongosi amewakumbusha wananchi kuwa CCM ina historia ndefu ya kuchukua hatua dhidi ya viongozi wasiowajibika, akiikumbusha mifano ya operesheni za kuwataka viongozi 'kuvua gamba' pamoja na kung'oka kwa waliowahi kuitwa 'mawaziri mizigo'.
"Ndani ya chama hiki hakuna mkubwa kuliko chama. Na hiyo ndio nidhamu ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa hiyo tunapokuja kufanya ziara hatuji kucheka au kutembea. Tunakuja kuangalia kile kilichoahidiwa kimekamilika kwa namna gani," amesisitiza Kihongosi