Kiingereza cha Diamond,The Sporah Show na kile cha Shigongo,Straight Talk Africa

you have a point.... it's best to focus kwa interview instead of kujichetua mpaka point ya interview inapotea watu wanaanza kuconcentrate na broken badala ya dhana ya kipindi

That is it
 
Shigongo alikuwa anajitaidi kuongea kimarekan ila alifanya vizuri am inspired

Anajitahidi kuongea na nimempongeza,issue inakuja anapotaka kujifanya yeye ni LeBron James au Shaquil O'neil
 
Shaka hawezi kuajiriwa BBC?na VOA anafanya nini
LAbda sijaeleweka. Na pengine sijaweka vizuri. Kuna ile kuwa official mtangazaji na kuwa mwandaaji wa kipindi fulani. Hata hapa kwetu (labda kwa hivi vituo vnavyoota kama uyoga) ni ngumu kumuweka mtu kuwa mrusha habari na ana lafudhi ya kabila fulani. Lazima kiswahili kinyooke. Pengine huyo mtu atakuwa ripota tu kama kina Maratu. Pengine kwa umuhimu wa huyo mtu kama ilivyo kwa Shaka, atapewa kusimamia kipindi fulani ila si kurusha habari
 

Fikria mkuu,wanaoangalia TV sio.wazungu ndo maana.kiswahili kilitumika ili audience wote waelewe kipi kinachoendelea kwenye mdaharo
 

Maratuuuuuu,haha...OK,nimekupata
 
Shigongo alipiga ngeli kali na alijiamini sana kiasi kwamba alianza kupoteza lengo kwa kutafuta misamiati ming isiyonasababu mfano alisema alikuwa Dumbest in school, hapa hata shaka hakuelewa alikuwa anamaanisha nini mpaka alitotumia maneno ya kawaida, hivyo naungana na mtoa mada kuwa wasipanie sana.
 
Yaani...:

1.Watu waongee Kiingereza kwa lafudhi za makabila yao au...?
2.Lafudhi ya Kiingereza ya Shaka Ssali iwe mfano wa kuigwa...?
3.Matamshi ya Kiingereza cha Ki-Nigeria kiwe cha kupigiwa mfano...?

Sifa ya lugha yoyote ile inahitaji sana utamkaji wa maneno kwa usahihi kama wazungumzaji asilia wa lugha husika.

Maoni yangu kwa uchache:
Ulipaswa kuwatia moyo. Shigongo amejieleza wazi kabisa yeye ni darasa la Saba.Lakiniwenye hiyo 'video clip" hapo juu anastahili pongezi. Na amejibu maswali yake sawa na alivyo ulizwa, sana tu....
 
Mahojiano ya membe yanahusu mambo ya kitaalam.. Mazungumzo ya diamond ni ya kawaida tofaut
lakini Membe si ni mtaalamu kwenye kazi anayoifanya, ilitakiwa amudu lugha ya kitaalamu kwenye hilo eneo kuliko hata ya mtaani. Unless unajaribu kutuaminisha hata huo utaalamu hana
 
Nimeangalia video ya Shigongo... ni kweli ingekuwa better kama asingetumia accent ya kimarekani, lkn kwa education level yake yake kama mlivyoielezea hapa, kutumia accent sio kitu cha ajabu.
All in all, amejitahidi sana. Ni mfano wa kuigwa kwa achievement yake. Tumpe support
 
Dah Mulugo yupo wapi? Dah yule mshikaji bana,,,tehe tehe
 

Mambo ya kumuita wife "He" huku anaweka accent ya kimarekani "you know, gonna"
 
lakini Membe si ni mtaalamu kwenye kazi anayoifanya, ilitakiwa amudu lugha ya kitaalamu kwenye hilo eneo kuliko hata ya mtaani. Unless unajaribu kutuaminisha hata huo utaalamu hana

Lugha ya kitaalamu na lugha ya mazungumzo ni tofauti
 

Kingereza na lugha zingine za watu wengine siyo ishu sana mkuu,,hakuna mahusiano kati ya kujua lugha na elimu ya mtu..tukipende Kiswahili chetu
 
Ivi hii kasumba ya kuongea kingereza itaisha lini hapa tz..tumekuwa brainwashed yani kwetu mtu anayejua kuzungumza kiingereza ndo msomi na aliyestaarabika...
 
Hata hivyo sio lugha yetu hata kama angeongea kisukuma au kimanyema na kutafuta wakalimani nisingewashangaa daima dawamu.......chukueni 5

utabaki kusema siyo lugha yetu wakati wengine wanatia bidii kujifunza na kuweza kungaa kimataifa. kujifunza kitu tofauti na ulicho nacho kunalipa. angalia Diamond anavyojitahidi hata anaweza kuongea na waandishi wa kimataifa bila mkalimali.
 
Ivi hii kasumba ya kuongea kingereza itaisha lini hapa tz..tumekuwa brainwashed yani kwetu mtu anayejua kuzungumza kiingereza ndo msomi na aliyestaarabika...
kweli hii kasumba inafanya watu wadharau cha kwao.sijui ni mfumo tuliojiwekea.ukienda kufanya interview mahali wakikuambia chagua kiswahili au kiingereza ninauhakika ukichagua kiswahili hupati kazi.wakati unaoenda kuwahudumia ni watu ambao hata kiingereza hawajui.ila kwa upande mwingine nivizuri kujua lugha nyingi kutokana na utandawazi.au ukiwa na plan za kufanya kazi kimataifa.hautakua na mkalimani kwa mfano ukiwa doctor hosp lazima ujue lugha ya hapo ya hiyo sehemu.ila tz lazima tubadilike.tunasujudu sana kiingereza bilasababu za msingi japo ni muhimu kukijua.
 
Anajitahidi kuongea na nimempongeza,issue inakuja anapotaka kujifanya yeye ni LeBron James au Shaquil O'neil
ingependeza zaidi wangeongea kiingereza lakini kwa accent ya kwao.kama waganda na wakenya.mbona poa tu.accent nikama the color of your skin you can do nothing about it.sikumoja mwal wangualisema kilamtu anaaccent na kilamtu anajua hivyo so tusione aibu kuongea.hatauifiche vip itajitokeza tu.hasa kwa sie tulio kijulia uzeeni.cha msingi watoto wetu waanzishiwe mapema kama hatutaki wawe na accent. za kihaya kwa kuwapeleka international schools au marekan na kwingineko kama hatutaki hizi vitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…