Kiingereza cha Rais Samia

Kiingereza cha Rais Samia

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza 🤣. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza 🤣. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

😂😂mwenzako hajakaa Marekani kama wewe mkuu,mtu wa Huku Kizimkazi katembea sana ni hapa Dar na Dodoma unataka kumuweka daraja sawa na mtu wa Cleveland,Salt lake,Idaho,wichita,New york na Atlanta?? Tumvumilie tu mkuu yatakwisha
 
Kuhusu facts ndogo ndogo nimewahi kuuliza wanao muandalia speech wanakuwaga na lengo Gani na yeye kwa nini huwa hazikagui,

Hofu yangu huyu bibi ni mvivu Fulani ni mtu wa kulishwa Kila kitu...

Nilishangaa na Mimi kusikia Kamala ndio mgombea wa kwanza mwanamke...

Kingine Samia siyo mtu wa kusikiliza na kutoa arguments, Bali wa Ndiyo ndiyo Kila unapomwabia kitu, nilisikia hii wakati Kamala anazungumza
 
Akisoma anakuwa fluent kidogo, kuwa mtu wa pwani kunamfanya aweze kusoma vizuri.

Yale ya kutoa kichwani ni mweupe pe! Kama mimi tu😋
Hapana.

Fluency haihusiani na kusoma vilivyoandikwa.

Ni kwamba hana lafudhi nzito/ nene. Hicho ndicho kinachomfanya aonekane ana afadhali.

Lakini maneno mengi sana yanampa shida kuyatamka.

Hata yale maneno ya kawaida ya hiyo lugha hawezi kuyatamka vizuri.

Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.
 
😂😂mwenzako hajakaa Marekani kama wewe mkuu,mtu wa Huku Kizimkazi katembea sana ni hapa Dar na Dodoma unataka kumuweka daraja sawa na mtu wa Cleveland,Salt lake,Idaho,wichita,New york na Atlanta?? Tumvumilie tu mkuu yatakwisha
Huyu alizaliwa na kukulia Butiama huko.

Hebu mcheki hapo. Super impressive.

Hasomi popote.

Kwangu lugha maridhawa si tatizo sana kwa sababu Umombo si lugha yetu mama, nakwazika sana Rais yoyote akiwemo Samia kuanza kukandia viongozi waliopita wakati ni viongozi waliotokana na chama kilekile kiitwacho chama tawala...

Sijui hawaelewi kuwa unapomponda Rais aliyepita ni sawa kabisa na kukiponda chama chao wenyewe na sera ama ilani zake...
 
Back
Top Bottom