Ngoja tuiweke katika mfano huu.
Wasanii wawili wanafanya shoo siku mbili tofauti.
Msanii mmoja ni mkubwa na mwingine ni mdogo anajitafuta.
Huyu msanii mkubwa katika hali tu ya kutazamia na kile ambacho ni rahisi kufikiri kutokana na ukubwa wake basi msanii huyu anategemewa kuwa na shoo yenye gharama kubwa sana.
Kwa gharama hizo kubwa kuanzia za kimaandalizi hadi mikakati basi msanii huyo hawezi kuwa na dau dogo la kiingilio kuliko msanii mdogo.
Msanii mdogo huyu shoo yake ipo low key utakuta mara nyingi kulingana na fanbase yake kuwa ndogo unakuta kiingilio ni bia.
Na hiyo bia sio hizi aina ya Hennesy ni hizi Sungura ambazo ni 1,500 na sometimes ili kuwafanya watu walau waingie unakuta host wa shoo anatangaza mademu kiingilio ni bure ili kuwavuta men.
Yanga ni aina ya msanii mdogo ambaye hana uhakika na mashabiki wake, wamefanya hivyo kwenye mechi ya Medeama na bado kulikuwa na muitikio hafifu wa watu kwenda uwanjani.
Na mind you, hiyo jumamosi lucha ya kwamba kiingilio ni bure ila usikute Yanga wwenyewe wakawa wakuhesabika na sehemu kubwa ya uwanja ikajazwa na mashabiki wa Simba.