Quinty
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 462
- 74
Bora leo nimekutana na watu ambao tunaudhika na tatizo moja. Nilikuwa nikijiuliza mara nyingi ni nini mantiki ya majina ya hizi filamu za kwetu kuwa na majina ya kizungu na matangazo ya kizungu na wakati ni za kiswahili na pia walengwa ni wanaotakiwa kununua na kwenda kuangalia ni waswahili. Nikweli huwezi jifunza bila kujaribu ila sasa hii imezidi kuna shule kede kede za kwenda kujifunza ni uigizaji na jinsi ya kutengeneza filamu. Hii habari ya kwamba watu wamezaliwa na kipaji inabidi tuiweke kando maana imeshaonekana kwetu Tanzania haina tija. Ndo maana unaangalia filamu mtu anahuzuni lakini haonekani kama ana huzuni nikiwa na maana kuuvaa uhusika halisi. Ndiyo maana hata filamu zetu huwezi angalia zaidi ya mara moja maana zinachosha. Waone wenzao kina Harrison Ford, Denzel Washington, Will Smitt, Ashton nk wamekwenda shule na wamezungukwa na timu inayojua nini cha kufanyika. Sasa sisi tumeng'ang'ania kila kitu muigizaji Kanumba/Ray, mwandishi, Mtayarishaji, Muongozaji, Mpiga picha huyo huyo mtu mmoja tutaweza wapi. Tukubali kwenda shule na kuongeza kiwango pia kubadili majina yaendane na filamu zenyewe...Siyo Student of Africa sijui white chair...haya mambo ya kuiga Nigeria waache.
