Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,933
- 988
Uamuzi wa kufunga Shule ya Sekondari ya Kibiti ulitoka na maamuzi ya Bodi ya Shule hiyo katika kikao chao walichofanya Jumatano ya 14/11/2012, na utekelezaji wake kufanyika Alhamisi ya 15/11/2012. Si kama mwanaJF mmoja aliyesema kuwa yalikuwa ni matakwa ya Mkuu wa shule. Kiuhalisia hali ya usalama shuleni hapo ilikuwa tete.
Mwanzo wa Tatizo.
Illikuwa ni siku ya Jumapili ya 11/11/2012 ambapo kuna baadhi ya wanafunzi ambao ni viongozi wa Chama cha wanafunzi wa kiislamu shuleni hapo (KIMSYA) walikwenda kwenye kongamano huko Kibaha na kurudi jioni majira ya saa moja usiku. Muda wa saa 5 usiku walipiga adhana (adhana inaweza kupigwa wakati wowote endapo kuna msiba wa kiongozi au kuna jambo la dharura limetokea). Wanafunzi wakiislamu wakaingia katika masjidi ilyopo shuleni na kufanya kikao ambacho viongozi wao walikuwa wakiwaeleza yale waliyojadiliana Kibaha na kuhakikisha nao wanafanya kile ambacho wenzao wa Bagamoyo na kwingine katika shule za pwani walifanya; kwa lugha yao wanasema kutoka katika ukandamizwaji unaofanywa na wakristo kupitia mfumo kristo . Hoja zao nyingine zilikuwa ni kuhakikisha panakuwa na usawa wa viongozi wa serikali ya wanafunzi (shuleni hapo HP ni mkristo, Vice HP ni mkristo, Secretary ni muislamu; wanataka kama HP akiwa mkristo basi Vice awe muislamu: walisahau kwamba viongozi hao walichaguliwa kwa kura za wanafunzi wote)
Pia waliazimia kwenda kumvamia na kumpiga Mkuu wa Shule usiku huo ikiwa ni namna ya kutimiza malengo yao ya kulianzisha soo . Mkuu wa shule akajulishwa juu ya mpango huo na majira ya sa saba ya usiku aliwaita viongozi wa KIMSYA na kutaka kujua madai yao. Ndipo baadaye akawaaambia mambo hayo watayajadili kwa kina kesho asubuhi yaani Jumatatu.
Ilipofika asubuhi aliwaita viongozi hao ofisini wakajadili hoja zao kwa kina moja baada ya nyingine. Katika hoja ya kuwa palikuwa na wanafunzi walibeba nyama ya nguruwe na kupeleka shuleni ilionekana ni uongo bali kilichotokea ni kuwa kuna wanafunzi waliondoka kwenda mtaani na kununua na kula nyama ya nguruwe huko huko kitaa; sasa baadhi ya wanafunzi wa kiislamu wakadai kuwa walitumia vyombo vyao kubebea nyama.
Utekelezaji wa Azma ya Uharibifu
Siku ya Jumanne asubuhi, Mkuu wa Shule akiwa katika mkusanyiko wa shule (school assembly) aliwaonya wanafunzi kutokujihusisha na vurugu zizote zenye mtazamo wa kidini ama kikabila ama kivikundi. Pia alionya wanafunzi wasiotaka kujifunza kuheshimu dini za wenzao; napengine kuanzisha chokochoko.
Hotuba hiyo haikuwafurahisha baadhi ya wanafunzi. Usiku wakati wengine wako wanasoma ilipigwa adhana wanaohusika walikwenda msikitini/masjidi. Huko wakapanga mikakati yao. Majira ya saa saba hivi ofisi za TYCS na CASFETA zilichomwa moto (inasadikiwa ni Petroli na kijinga cha moto vilitumika) kijinga cha moto kilipatikana katika dirisha la ofisi ya CASFETA. Wanafunzi walioshituka mapema kutokana na moshi uliotokana na kuungua kwa ofisi hizo ndiyo waliokimbia na kwenda kufanya juhudi ya kuuzima moto kabla hata ofisi na vyumba vingine havijashika moto uliokuwa unasambaa.
Wanafunzi wengi hawakuweza kulala usiku huo kutokana na hali kuwa tete na usalama kuwa mashakani.
Jumatano asubuhi, walifika Polisi na watu wa usalama kuja kuchunguza hali halisi ya mabo yaliyotokea. Kwa upande wa pili walimu nao walifanya jitihada zao katika kuweka shule katika hali ya usalama. Katika upekuzi waliofanya waalimu kwa kuingia katika ofisi zote za vyama vya kidini (wakati huo wanafunzi wote wako assembly ground) waligundua visu 10 katika ofisi ya KIMSYA,visu kadhaa mabweni, panga 1 na mafyekeo 2. Pia iligundulika kuwa ofisi ya KIMSYA inatumika kuwafindishia wanafunzi karate.
Katika siku hiyo hiyo, Bodi ya Shule ilikaa na kujadili hali ya Usalama hapo shuleni. Ambapo viongozi wa vyama vyama vya kidini na wale wa serikali ya wanafunzi wakiisha kuhojiwa na Polisi toka mchana hadi jioni waliiitwa pia kuhojiwa na Bodi ya Shule. Bodi ndipo, baada ya mchakato mrefu ikafikia uamuzi wa kuifunga Shule.
Usiku wa kuamkia Alhamis, wako wanafunzi walioendelea na vikao vyao na kupanga mkakati wa kufanya uharibifu wakiweka msimamo iweje wenzao kwingine wameweza wao washindwe. Haiwezekani Hata hivyo inatajwa kuwa kuna mwalimu wao ambaye alikuwa akilifahamu hili swala, aliwaonya sana kuwa wasifanye siku hiyo kwasababau usiku ule kulikuwa na watu wengi wa usalama.
Alhamisi asubuhi yapata kama saa mbili kasoro wanafunzi wakatangaziwa kuwa shule imefungwa kwa muda usiojulikana, watapewa taarifa ya kufungua shule baadaye, ili kupisha uchunguzi zaidi.Na kwamba wanapewa muda wa masaa mawili tu kujianda na kuondoka. Baada ya hapo hatakiwi mwanafunzi yoyote kuwepo shuleni hapo.
Matatizo mengine:
Yapo matatizo kadhaa ambayo yamekuwa yakizimwa kwa style ya kuvumiliana:
Source: Wanafunzi wa shule hiyo na mfanyakazi.
My take:
Tunaipeleka wapi Tanzania kwa kuwajazia watoto chuki na ubaguzi kwa misingi ya kidini?

- Discussion group zinafanywa kwa misingi ya kidini; wako wengi wa vijana wa kiislamu hawataki kuchangamana na wakristo.
- Kuna tanki la maji shuleni hapo ambalo wanafunzi wakristo hawaruhusiwi kuchota maji; kama haitoshi kuna upande maalumu unakaa ndoo za wanafunzi wa kiislamu.
- Kuna mabweni yamegeuzwa ni ya waislamu, mkristo haatakiwa kulala katika mabweni hayo (si utaratibu wa shule bali kuna wanafunzi wameutengeneza mfumo huu.