KIINI CHA KUFUNGWA SHULE YA SEKONDARI KIBITI (Vurugu zenye mlengo wa kidini)

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,933
Reaction score
988
Uamuzi wa kufunga Shule ya Sekondari ya Kibiti ulitoka na maamuzi ya Bodi ya Shule hiyo katika kikao chao walichofanya Jumatano ya 14/11/2012, na utekelezaji wake kufanyika Alhamisi ya 15/11/2012. Si kama mwanaJF mmoja aliyesema kuwa yalikuwa ni matakwa ya Mkuu wa shule. Kiuhalisia hali ya usalama shuleni hapo ilikuwa tete.

Mwanzo wa Tatizo.
Illikuwa ni siku ya Jumapili ya 11/11/2012 ambapo kuna baadhi ya wanafunzi ambao ni viongozi wa Chama cha wanafunzi wa kiislamu shuleni hapo (KIMSYA) walikwenda kwenye kongamano huko Kibaha na kurudi jioni majira ya saa moja usiku. Muda wa saa 5 usiku walipiga adhana (adhana inaweza kupigwa wakati wowote endapo kuna msiba wa kiongozi au kuna jambo la dharura limetokea). Wanafunzi wakiislamu wakaingia katika masjidi ilyopo shuleni na kufanya kikao ambacho viongozi wao walikuwa wakiwaeleza yale waliyojadiliana Kibaha na kuhakikisha nao wanafanya kile ambacho wenzao wa Bagamoyo na kwingine katika shule za pwani walifanya; kwa lugha yao wanasema ‘kutoka katika ukandamizwaji unaofanywa na wakristo kupitia ‘mfumo kristo’ ”. Hoja zao nyingine zilikuwa ni kuhakikisha panakuwa na usawa wa viongozi wa serikali ya wanafunzi (shuleni hapo HP ni mkristo, Vice HP ni mkristo, Secretary ni muislamu; wanataka kama HP akiwa mkristo basi Vice awe muislamu: walisahau kwamba viongozi hao walichaguliwa kwa kura za wanafunzi wote)

Pia waliazimia kwenda kumvamia na kumpiga Mkuu wa Shule usiku huo ikiwa ni namna ya kutimiza malengo yao ya kulianzisha soo . Mkuu wa shule akajulishwa juu ya mpango huo na majira ya sa saba ya usiku aliwaita viongozi wa KIMSYA na kutaka kujua madai yao. Ndipo baadaye akawaaambia mambo hayo watayajadili kwa kina kesho asubuhi yaani Jumatatu.

Ilipofika asubuhi aliwaita viongozi hao ofisini wakajadili hoja zao kwa kina moja baada ya nyingine. Katika hoja ya kuwa palikuwa na wanafunzi walibeba nyama ya nguruwe na kupeleka shuleni ilionekana ni uongo bali kilichotokea ni kuwa kuna wanafunzi waliondoka kwenda mtaani na kununua na kula nyama ya nguruwe huko huko kitaa; sasa baadhi ya wanafunzi wa kiislamu wakadai kuwa walitumia vyombo vyao kubebea nyama.

Utekelezaji wa Azma ya Uharibifu
Siku ya Jumanne asubuhi, Mkuu wa Shule akiwa katika mkusanyiko wa shule (school assembly) aliwaonya wanafunzi kutokujihusisha na vurugu zizote zenye mtazamo wa kidini ama kikabila ama kivikundi. Pia alionya wanafunzi wasiotaka kujifunza kuheshimu dini za wenzao; napengine kuanzisha chokochoko.

Hotuba hiyo haikuwafurahisha baadhi ya wanafunzi. Usiku wakati wengine wako wanasoma ilipigwa adhana wanaohusika walikwenda msikitini/masjidi. Huko wakapanga mikakati yao. Majira ya saa saba hivi ofisi za TYCS na CASFETA zilichomwa moto (inasadikiwa ni Petroli na kijinga cha moto vilitumika) kijinga cha moto kilipatikana katika dirisha la ofisi ya CASFETA. Wanafunzi walioshituka mapema kutokana na moshi uliotokana na kuungua kwa ofisi hizo ndiyo waliokimbia na kwenda kufanya juhudi ya kuuzima moto kabla hata ofisi na vyumba vingine havijashika moto uliokuwa unasambaa.

Wanafunzi wengi hawakuweza kulala usiku huo kutokana na hali kuwa tete na usalama kuwa mashakani.

Jumatano asubuhi, walifika Polisi na watu wa usalama kuja kuchunguza hali halisi ya mabo yaliyotokea. Kwa upande wa pili walimu nao walifanya jitihada zao katika kuweka shule katika hali ya usalama. Katika upekuzi waliofanya waalimu kwa kuingia katika ofisi zote za vyama vya kidini (wakati huo wanafunzi wote wako assembly ground) waligundua visu 10 katika ofisi ya KIMSYA,visu kadhaa mabweni, panga 1 na mafyekeo 2. Pia iligundulika kuwa ofisi ya KIMSYA inatumika kuwafindishia wanafunzi karate.

Katika siku hiyo hiyo, Bodi ya Shule ilikaa na kujadili hali ya Usalama hapo shuleni. Ambapo viongozi wa vyama vyama vya kidini na wale wa serikali ya wanafunzi wakiisha kuhojiwa na Polisi toka mchana hadi jioni waliiitwa pia kuhojiwa na Bodi ya Shule. Bodi ndipo, baada ya mchakato mrefu ikafikia uamuzi wa kuifunga Shule.

Usiku wa kuamkia Alhamis, wako wanafunzi walioendelea na vikao vyao na kupanga mkakati wa kufanya uharibifu wakiweka msimamo “ iweje wenzao kwingine wameweza wao washindwe. Haiwezekani” Hata hivyo inatajwa kuwa kuna mwalimu wao ambaye alikuwa akilifahamu hili swala, aliwaonya sana kuwa wasifanye siku hiyo kwasababau usiku ule kulikuwa na watu wengi wa usalama.

Alhamisi asubuhi yapata kama saa mbili kasoro wanafunzi wakatangaziwa kuwa shule imefungwa kwa muda usiojulikana, watapewa taarifa ya kufungua shule baadaye, ili kupisha uchunguzi zaidi.Na kwamba wanapewa muda wa masaa mawili tu kujianda na kuondoka. Baada ya hapo hatakiwi mwanafunzi yoyote kuwepo shuleni hapo.

Matatizo mengine:
Yapo matatizo kadhaa ambayo yamekuwa yakizimwa kwa style ya kuvumiliana:

  1. Discussion group zinafanywa kwa misingi ya kidini; wako wengi wa vijana wa kiislamu hawataki kuchangamana na wakristo.
  2. Kuna tanki la maji shuleni hapo ambalo wanafunzi wakristo hawaruhusiwi kuchota maji; kama haitoshi kuna upande maalumu unakaa ndoo za wanafunzi wa kiislamu.
  3. Kuna mabweni yamegeuzwa ni ya waislamu, mkristo haatakiwa kulala katika mabweni hayo (si utaratibu wa shule bali kuna wanafunzi wameutengeneza mfumo huu.

Source: Wanafunzi wa shule hiyo na mfanyakazi.

My take:
Tunaipeleka wapi Tanzania kwa kuwajazia watoto chuki na ubaguzi kwa misingi ya kidini?
 
kazi ipo,nitarudi baadae

Umeona uzito wake mkuu!!

Kuikata mizizi ya huu mti wa udini uliopandwa na watu kadhaa waliokuwa wakizirusha mbegu zao zake si kitu rahisi.
Je walipanda wakijua ni matokea yake au bila kujua ni matokeo yake hili ni swali jingine zito zaidi.
 
"Hao siyo Waislam. Ni genge la Wahuni Wachache".
Hayo ndiyo majibu utakauoyasikia kutoka kwa viongozi wao wanaowatuma. Ukweli ni kwamba ninui Waislam pigeni shule acheni hizo tabia za kigaidi.

Amini Amini nawambia; Wakristo wana skili sana. Hawajibu mapigo kwa kuongea ongea wala kupiga matakbiri kama tunayopiga sisi. Wenyewe wako kimya kimya lkn wanendesha serikali za dunia hii. Jamani tule shule njia zetu za kudai haki ziko rudimentally and mechanical mno. Abgalieni hata kule Gaza wenzetu HAMASI wa.apiga makelele kama haya ya kwetu lkn Wayahudi kimya kimya wanatukamua damu na roho.

Angalieni hapa Tz kwa sasa. Ponda na mwenzie mandevu wamo wapi?
 
in short waislam hawapendi shule.. Nakumbuka zogo kama hili lilitokea minaki .. Wakafukuzwa shule sasa .. Wengi ni washakaji zangu nawaona wanaendesha boda boda sasa hivi.. Mmoja yeye mwislam ila hakupenda kufuata wenzake sasa hivi ni mwalim pale UDOM kwenye chuo cha waapemba
 
Umeona uzito wake mkuu!!

Kuikata mizizi ya huu mti wa udini uliopandwa na watu kadhaa waliokuwa wakizirusha mbegu zao zake si kitu rahisi.
Je walipanda wakijua ni matokea yake au bila kujua ni matokeo yake hili ni swali jingine zito zaidi.

Mkuu yani acha tu,hii mbegu ya udini inatuvuruga sana kwa sababu ya upumbavu wa watu wachache kwa tamaa zao za madaraka
 

Kutokupenda shule ndiyo iwe tiketi ya kupandikiza mbegu ya chuki kwa vijana wao?
Kutokupenda shule ndiyo iwe tiketi ya kuwachukia wenzao?
Kutokupenda shule ndiyo iwe tiketi ya kuwazuia wengine wasitumie fursa hiyo ya kuwapo shuleni?

Watafaidika nini kutokana na kupanda mbegu hizi?
Ni jamii gani katika ulimwengu wa leo inaweza kuendelea bila shule?

Kwanini serikali inawanyamazia kimya wapanda mbegu za chuki kwa wanafunzi?
Ni nani aliyeweka masharti hayo ya tanki la maji watumie wanafunzi wa dini fulani tu? Mbona wengine hatukusoma hivyo?

Mkuu najikuta ni maswali lukuki.
 
MNYAMAHODZO kwanza nikupongeze kwa mambo mawili, moja ni kwamba jina lako na avatar yako vimesadifu kwelikweli,safi sana. Pili, wewe ni mwandishi mzuri sana,umeiandika stori hii vizuri sana kimtiririko na it seems you are well informed na hubahatishi.
Maoni yangu ni kwamba pamoja na ukweli kwamba shule imefungwa kupisha shari na kuruhusu uchunguzi zaidi kufanywa,naona haki haijatendeka sana.wale viongozi waliohudhuria kongamano kule kibaha ndio walitakiwa washughulikiwe kama akina PONDA, FARID na wengine lakini wakristo wapewe fursa ya kuendelea na masomo kwani wao siyo waliopanga vurugu hizo.lakini pia wapo waislamu wazuri tu tena wengi wanaopenda kusoma na kufikia malengo yao,walindwe wasome na wajiandae kwa mitihani ya kidato cha sita.
 
visu na mapanga ili kupunguza mfumo kristo, kutenganisha maji yao na ya mfumo kristo, ili waweze kuhujumu mfumo kristo, washauri wao wazee/wazazi wao ambao hawakwenda shule, na hali zao mbaya, sasa ili nao wapate nafasi ni kuhujumu mfumo kristo, halafu baada ya hapo watasema wapewe nafasi zaidi za kazi za juu? na kwenye timu zetu za mpira tutaanza kuangalia mfumo kristo wangapi na wasafi ni wangapi, mwishowe tutakuja na wazo wachezaji hawa walale kufuatana na imani zao na walimu wao wao ni kutokana na imani yao, kwani kafiri kumfundisha msafi, ni kumchafua msafi na kumtia najisi, leo katika picha za mkutano wa ccm zanzibar, nimeona wafuasi hao wakishangilia kwa staili moja ambayo ina najisi usafi wa wanaume/wanawake wa huko, pia kwenye picha za matukio nimeona Hawa Ghasia waziri akiongea na mfanyakazi wa wizara yake ambaye ni mwanaume, hii naona si haki ni kumchafua mtu msafi , basi madai yetu yataendelea na kuendelea, mwishowe nitabaki mimi mimi peke yangu nilie msafi.
 
.....kwanza wakati wanafunzi wanatenganisha mabweni ya waislamu na dini nyingine, wanatenganisha matenki na dini nyingine walimu na uongozi wa shule ulikuwa wapi? Hapo wao ndo wamezembea, huu ujinga huwa unaanza kidogo kidogo kisha unaota mizizi

pili hao magaidi wachukuliwe hatua, yes huo ni ugaidi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu, warudi mtaani wakajifunze maisha ni nini............ Hapo unaweza kuta wanafunzi wenyewe wanatoka kwenye familia za tia maji yia maji (ndo maana wapo shule za kata) ila wanaendekeza ujinga wa kidini, badala ya kusoma wakomboe familia zao na dimbwi la umasikini.....

Halafu wakati wakijifunza karete hapo walimu walikuwa wapi?

Kuna udhaifu mkubwa na upande wa walimu pia.......

Mwisho hivyo vyumba vya ofisi wote wanyang'anywe kuanzia ycs,ukwata, wapagani, waislamu, na dini nyingine, mipango yote ya kidini ifanyike madarasani......

Mabweni wapange upya tena zoezi lifanyike kwa umakini.....

Bika kusahau hao walojaribu kuchoma moto wachukuliwe hatua za kisheria, imagine moto ungeshika shule nzima, madhara yake yakoje?

Na hivyo visu wanamatumizi nayo gani?


 
..kama kweli polisi wanataka kufuatilia hilo hao wanafunzi wabanwe huko.walikokuwa kwenye kikao na kupandikizwa mbegu za vurugu, huo utakuwa mwanzo mzuri wa kuwakamata wahusika.....hayo ni kama tu kweli serikali ya ccm ipo serious na kukata mbegu yake iloipanda.............
 
Hao waislamu hawana jipya wanapenda sana vurugu pumbavu sao sana
 
Mie nafikiri suluhisho ya haya yote ni kuufunga ubalozi wa Iran,ndio uko nyuma ya ivi visa.
 
Hao waislamu hawana jipya wanapenda sana vurugu pumbavu sao sana

Kushambulia kwa maneno makali au kutukana hakusaidii.

Mti huu wa chuki za kidini unakua, tena kwa kasi. Tukifikiri kuukata wenyewe, tujue utachipuka maadam mizizi ipo. Jambo la muhimu kuitafuta mizizi na kuikata. Mti huu nao utakufa kwa kunyauka.
 
Hateful Speeches at work

Who has delivered the hateful speech?

Or

Who is delivering the hateful speech?

Do you the outcome of keeping under the blanket on what had happen at Kibiti Secondary?
Tell us, in detail, what is the difference with what had happened at Bagamoyo Secondary School the previous month?
 
Hii dhambi sasa inaota mizizi, la kuogopa ni kuwa hata wale wasiokuwa na chembe za udini sasa wanaanza kujihisi wao ni either wakristo au waislamu, ndugu zangu CCM kwa kutaka kura za 2010 mmetufikisha pabaya.
tatizo si ccm.ccm na kura vinahusika je hapa! tatizo ni baadhi ya wanadini wakiwemo watu wa jamii ya akina PONDA AMBAO WANAENEZA CHUKI ZA KIDINI NA KUANZISHA WANACHOKIITA KUPINGA MFUMO KRISTO AMBAPO DHANA AMBAYO WAMEKUWA WAKIIFUNDISHA NI KUWATAFSRI WAKRISTO,SERIKALI NA TAASISI ZAKE KAMA MAADUI HIVYO KUPINGA KILA KILICHO CHAO KWA VYOVYOTE ITAKAVYOWEZEKANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…