Kijana ajiandikia R.I.P kabla ya kujiua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Dennis Yego (24) alimchoma visu mkewe na akajinyonga. Jumatatu saa mbili na dakika tano usiku, aaliandika “Rest in peace to me” kwenye ukurasa wake wa facebook. Dakika kadhaa baadae akaandika, kama unanidai nione kabla ya mchana wa kesho

Walter Teno mwenyekiti wa eneo hilo alisema kijana huyo alimfuata kwa kuwasuluhisha kwa ugomvi aliokuwa nao na mkewe

Mwenyekiti ameshangazwa na tukio hilo kwa kuwa alidhani waliyamaliza. Alisema kijana huyo alimpiga mkewe visu vingi lakini hakufa kwa sasa yupo hospitali ya rufaa ya Kapsabet

Kamanda wa polisi alisema walikuta mwili wa kijana huyo kwenye mti na kijana huyo hakuacha waraka wowote

Chanzo: Daily Nation
 
Vijana wasipo mtafuta yesu wataendelea kuisoma namba maisha yao yote

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hadi hapo alipofikia maamuzi ya kujitoa uhai hakuwa amemtafuta Yesu? Yesu alikuwa chombo tu, MWANA wake Mungu. Ingekuwa waliomjua kwa undani, majirani na marafiki zake walikuwa wanafata mafunzo ya Yesu wangekuwa wamemnusuru kabla hajazamia kwenye shimo hilo la giza. Ukweli ni kwamba viongozi wa kidini na makanisa kwenye nyakati hizi sio hifadhi tena kwa vijana, sana sana wanaopitia mateso na wakati mgumu maishani. Siku hizi watu wanaenda makanisani kuwaombea mabaya 'maadui' zao na kuringiana kwamba nimebarikiwa zaidi ya yule. Badala ya kueneza upendo kote kote kwa wasiojiweza, wanaobeba mizigo mizito, mayatima n.k. n.k. Nikisikia mtu anakuja kwa jina la Yesu siku hizi huwa nampa kisogo na nakaa mbali naye.
 

R.I.P baaria though naona ilikuwa mission impossible coz manzi bado anavuta punzi
 
Unataka watu waje kwa jina gan?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waje kwa matendo yao sio jina, .....na kwa matendo yao tutawajua. Yaani imeandikwa hadi kwenye kitabu kitakatifu. Wazee wa ndemi na mathati nao wakasema kwamba chema chajiuza na kibaya chajitembeza.
Hujui hata kwa matendo yako bila Yesu Kristo ni kazi bure tu au hujui

Hujui kama penye uzima,penye ushindi ni palimo krsto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…